Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Sado
Shija (45) Mkazi wa Kata ya
Sibwesa Tarafa ya Mwese Wilaya ya Mpanda
Mkoani hapa ameuwawa kikatili kwa kukatwakatwa na mapanga na watu watatu wasio fahamika huku watoto wake wakiwa wanashuhudia
mauwaji hayo
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio hilo la mauwaji ya kinyama na
yakusikitisha yalitokea hapo juzi majira
ya saa mbili na nusu usiku nyumbani kwa
marehemu
Alisema siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa amekaa nyumbani kwake nje
akiwa na watoto wake watatu ambao
ni Shinje Italam(25) Mbuke Italam(10) na
Ikollo Italam(7) huku wakiwa wanaota moto baada ya
kumaliza kula chakula cha usiku
Ndipo ghafla
walitokea watu watu watatu
wasiofahamika huku wakiwa na tochi ambazo walizitumia kuwamulika na mikononi wakiwa na mapanga na walibisha
hodi kwa lugha ya Kabila la Kisukuma
Alisema
kisha watu hao walianza kumshambulia mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye
Shinje kwa kumpiga na fimbo kwenye sehemu
mbalimbali za mwili wake hari
ambayoilimfanya akimbie mbio na kumwacha marehemu na wadogo zake hata hivyo
mmoja wa watu hao alimkimbiza lakini
hakufanikiwa kumkamata
Kidavashari alieleza
kuwa watu wawili waliokuwa wamebaki walianza kumshambulia marehemu kwa kumkatakata
kwa mapanga huku watoto wake wakiwa wanashuhudia hadi baba yao alipofariki Dunia
Alisema marehemu wakati wa uhai wake kabla haja hamia kwenye kijiji hicho alikuwa
akiishi huko katika kijiji cha Usevya T
arafa ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele pamoja
na mke wake mkubwa aitwaye
Mwanamlekwa Italam na siku za
nyuma aliwahi kuandikiwa barua mara nne za kumtishia
kuwa asipo hama kwenye kwenye nyumba
ambayo walikuwa wakishi na
mke wake mkubwa
atauwawa kwa kukatwa na mapanga
Kamanda
alieleza Inasadikiwa barua hizo
za vitisho zilikuwa zimeandikwa na
shemeji wa marehemu aitwaye
Nyandaco Giduja
Alisema watu wawili ambao ni watoto wa marehemu Shinje
Italam 25 na Shile Italam wanashikiliwa na jeshi la polisi
kwa tuhuma za mauwaji hayo ambao
wanadaiwa walikuwa na ugomvi na baba yao wa
kugombea ng’ombe 20 walizokuwa wanadai zilitolewa kama mahari za dada
yao wakati alipokuwa akiolewa madai
ambayo yalikuwa yakiungwa mkono na shemeji ya marehemu
Kamanda Kidavashari alieleza watuhumiwa wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote
mara baada ya uchunguzi wa tukio
hilo utakapo kuwa umekamilika
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment