Na Walter
Mguluchuma Katavi
Watu wawili
Charles Gerald Ngonyani(38) Mkazi wa Kijiji cha Uruwila Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi na Geofrey
Ngonyani (22) Mkazi wa Mkoa wa Mwanza
wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kukamatwa
na meno ya Tembo vipande 20 yenye uzito
wa kilo 61 yenye thamani ya Tsh Milioni 90 wakati wakiyasafirisha kwenye basi
la Kampuni ya Adventure Conection
Kwa mujibu wa Kamanda wa jeshi la Polisi wa
Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari watuhumiwa hao walikamatwa hapo Oktoba 11
mwaka huu majira ya saa nane na nusu mchana katika eneo la stendi kuu ya mabasi
ya Mpanda mjini katika Mtaa wa mji mwema
Alisema
watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa
wamepakia meno hayo ya Tembo kwenye basi la kampuni ya Adventure Conection
lenye Namba za usajiri T 792 ALF aina ya
Scania lenye makao yake makuu Mkoani
Kigoma linalofanya safari zake kutoka Mkoa wa Katavi kwenda Kigoma
Kidavashari
alifafanua watuhumiwa hao walikamatwa
na meno hayo ya Tembo ambayo walikuwa wameyaficha kwenye Buti la Basi hilo na mengine kwenye kelia huku wakiwa wameyahifadhi ndani
ya mabeji matano ya salifeti
Alisema
siku hiyo ya tukio majira ya saa
sita mchana jeshi la polisi walipata
taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna
watu watatu watasafirisha meno ya Tembo
kutoka Mkoani Katavi na kuyasafirisha kuyapeleka Mkoani Kigoma kupitia
kampuni ya basi ya Adventure Conection
Alieleza baada ya polisi kuwa wamepata taarifa
hizo waliandaa mtego wa kuwakamata watuhumiwa hao katika eneo hilo la stendi ya
Mabasi
Alifafanua watuhumiwa hao walifika kwenye eneo la stendi
na kupakia meno hayo ya tembo kwenye
buti la gari beji tatu za aina ya
salifeti na beji mbili nyingine
waliziingiza ndani ya basi kwa kupitia
kwenye dirisha la basi huku muda wote huo polisi wakiwa kwenye mtego wa kuwakamata
Alisema
watuhumiwa hao walikuwa wakishirikiana
na mwenzao mmoja aliye fahamika kwa jina la John Kajuti ambae alifanikiwa kutoroka mara baada ya kuona wenzake wamekamatwa
Jeshi la polisi
linaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo ambae aliyetoroka ili
aweze kuunganishwa na wenzake kujibu mashitaka yanayo wakabili
Kamanda
Kidavashari alisema watuhumiwa hao wawili waliokamatwa wanatarajiwa kufikishwa
mahakamani ili waweze kujibu mashitaka
yao ya kupatikana na nyara za Serikali
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment