Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkuu wa
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Paza
Mwamlima amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda
na wa Mji wa Mpanda kuhakikisha wanatekeleza agizo lake alilolitoa la
kuwasaka na warudisha mashuleni wanafunzi wote walioacha masoma na kukimbilia
kuolewa na kuowa
Mwamlima alitowa
maagizo hayo ya kuwataka wakurugenzi walioko kwenye Wilaya yake watekeleze
maagizo yake hapo juzi wakati akiwa
ofisini kwake kwenye kikao chake na wakurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda na Mji wa Mpanda
kikao hicho kiliwashirikisha wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Wilaya ya Mpanda
Alisema
kumekuwepo na tatizo kubwa la
wanafunzi kukatisha masomo kwa
lengo la kuolewa na wengine kwa ajiri ya kuowa kitendo hicho ambacho
hakitakiwi
Alifafanua
kutokana na kushamiri kwa utoro wa wanafunzi
alilazimika kutowa agizo
hapo mwezi mei mwaka huu wakati alipofanya ziara kwenye
shule ya Sekondari ya Mpanda Ndogo alipokuta zaidi ya nusu ya wanafunzi wa shule hiyo walikuwa wameacha
masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya wanafunzi kuolewa
Wakati wa
ziara yake hiyo alishitushwa na taarifa ya kutoripoti shuleni
wanafunzi wawili wa shule ya Msingi Vikonge ambao waliongoza kwa matokeo ya
ufaulu wa mtihani wa kumaliza Darasa la
saba mwaka jana lakini wameshindwa kujiunga na kidato cha kwanza katika
Sekondari ya Mpanda Ndogo
Dc Mwamlima
kwenye ziara hiyo aliwaagiza wazazi wa wanafunzi walioacha masomo wahakikishe wanawarudisha
shuleni watoto wao hata kama wameulewa na kuzaa watoto
Pia aliwaagiza
wakurugenzi hao wahakikishe wanafanya kikao cha pamoja baina ya Halmashauri
hizo na
Hifadhi ya Taifa ya Katavi na
Vijiji vinavyozunguka hifadhi ili kuonyesha mipaka kwa lengo la kuondoa migogoro baina ya vijiji na Hifadhi
Aidha
amewaagiza waandae kikao
cha pamoja cha wadau wa mto
Katuma ili waweze kujadili na kupanga mikakati ya kuunusuru mto
huo usikauke ambao ni tegemeo la wanyama
waliooko kwenye Hifadhi ya Katavi
Amewaagiza
vilevile wamalize ujenzi wa maabara kabla
ya mwezi wa tisa mwaka huu ili
nayeye aweze kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa
Katavi ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais alilolitowa la kila shule ya
Sekondari hapa Nchini lazima iwe na jengo la maabara
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Home »
» DC MPANDA AWAAGIZA WAKURUGENZI KUTEKELEZA MAAGIZO YAKE
0 comments:
Post a Comment