Home » » DC AKAZIA AGIZO LAKE

DC AKAZIA AGIZO LAKE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

MKUU wa Wilaya (DC) ya Mpanda mkoani Katavi, Paza Mwamlima amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za Mpanda na Mji wa Mpanda kuhakikisha wanatekeleza agizo lake la kuwasaka na warudisha shuleni wanafunzi walioacha masoma na kuozwa.
Mwamlima alikazia agizo hilo juzi wakati akizungumza na wakurugenzi hao katika kikao kiliwashirikisha wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama  wa wilaya ya Mpanda.
Alisema kuwa kumekuwepo na tatizo kubwa la wanafunzi  kukatisha masomo kwa lengo la kuolewa na wengine kwa ajiri ya kuowa, jambo alilosisitiza kuwa ni makosa.  
Alisema kuwa Mei mwaka huu,  alifanya ziara kwenye shule ya sekondari ya Mpanda Ndogo ambapo alikuta zaidi ya nusu ya  wanafunzi wameacha masomo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kuolewa.
Katika ziara hiyo, aliwagiza wazazi wa wanafunzi  walioacha masomo wahakikishe wanawarudisha shuleni watoto wao hata kama wameolewa na kuzaa.
Pia aliwataka wakurugenzi hao wahakikishe wanafanya kikao cha pamoja baina ya halmashauri hizo  na Hifadhi ya Taifa ya Katavi  pamoja na vijiji vinavyozunguka hifadhi ili kuonyesha mipaka kwa lengo la kuondoa migogoro baina ya vijiji na Hifadhi.
Mkuu huyo, pia aliwaagiza wakurugenzi hao waandae kikao cha pamoja cha wadau wa mto Katuma  ili waweze kujadili na kupanga mikakati ya kuunusuru mto huo usikauke kwa kuwa ni tegemeo la wanyama wa Hifadhi ya Katavi.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa