Home »
» HOT NEWS: MHUDUMU WA AFYA JELA MIAKA MITATU KWA KUPOKEA RUSHWA YA TSH 25,000
HOT NEWS: MHUDUMU WA AFYA JELA MIAKA MITATU KWA KUPOKEA RUSHWA YA TSH 25,000
Jiunge na Huduma ya Tone Mobile News Bure kabisa kupitia Whatsapp yako na uwe wa kwanza kupata kile kinachotokea ni Rahisi sana Ingia katika uwanja wa kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika Whatsapp yako kisha andika TONE MOBILE NEWS tuma kwenye namba 0756364660 utapokea ujumbe kuwa umeunganishwa.
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda imemuhukumu mhudumu wa Afya wa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Peter Nyirenda kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kuomba na kupokea Rushwa ya Tsh 25,000
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya mahakama kulidhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka na utetezi
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Bahati Haule aliileza mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo hapo julai 15 mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda
Alidai kuwa siku hiyo ya tukio mshitakiwa akiwa mhudumu wa Afya katika wodi ya watoto katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda aliomba na kupokea kutoka kwa msiri iliaweze kumpatia matibabu mtoto wake aliyekuwaamelazwa katika wodi ya watoto katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda
Mwendesha mashitaka Haule alieleza baada ya taarifa kufikishwa TAKUKURU waliandaa mtego na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa siku hiyo ya tarehe 15 Julai mwaka huu
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU alimsomea mshitakiwa mawili ambayo ni kuomba Rushwa ya Tsh 25,000 na kupokea Rushwa ya Tsh 25,000 kinyume na matakwa ya mwajiri wake kinyume na kifungu cha sheria cha 15 (1)(a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007
Mshitakiwa Peter Nyirenda baada ya kusomewa mashataka hayo mbele ya Hakimu Chiganga Ntengwa alikiri mahakamani kutenda kosa hilo la kuomba na kupokea Rushwa
Hakimu mkazi Chiganga Ntengwa aimtaka mshitakiwa kabla ya kutolewa kwa hukumu kama anayosababu yoyote ya msingi ya kuiomba mahakama impunguzie adhabu aieleze mahakama ambapo mshitakiwa aliomba mahakama isimpe adhabu kwa kuwa ndio kosa lake la kwanza kufikishwa mahakamani
Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU Bahati Haule alipinga vikali utetezi huo kwa kile alidai kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi ya kuhusiana na Rushwa kutoka Idara ya afya katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na yanaathari kubwa kwa jamii kwani hugharimu uhai na afya ya mgonjwa
HakimuChiganga akisoma hukumu hiyo alisema mtuhumiwa baada ya kupatikana na hatia hiyo mahakama inamuhukumu kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya shilingi Tsh 500,000 hata hivyo mtuhumiwa aliweza kulipa faini hiyo na kunusulika kwenda jela
Pia hakimu Chiganga aliiambia mahakama kuwa hakuna kumbukumbu zozote ambazo zinaonyesha mshitakiwa kuwahi kutenda kosa hilo na mshitakiwa katika kesi hiyo hakuweza kuisumbua wala kuipotezea muda mahakama kwa kitendo chake cha kukiri kosa
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment