Na Walter Mguluchuma
Mpanda- Katavi yetu BlogWATU wawili wamekufa papo hapo na wengine 32 wamejeruhiwa vibaya huku mmoja wao akiwa amevunjika miguu yote miwili baada ya gari walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka .
Ajali hiyo ya barabarani ilitokea katika miteremko ya Mlima Sijonga katika barabara inayounganisha Mji wa Mpanda na Kijiji cha Karema mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Mpanda .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi , Focus Malengo akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu kutoka mjini Mpanda amedai ajali hiyo ilitokea Ijumaa , saa nne usiku katika Mlima Sijonga ikihusisha gari aina ya Fuso yenye nambari za usajiri T 759 FMU mali ya Ezekiel Molel (49) mkazi wa Mtaa wa Kawajense mjini Mpanda .
Alimtaja mmoja wa marehemu kuwa ni Hamadum Neema (34) mfanya biashara wa mjini Mpanda ambapo mwingine bado hajatambuliwa ila anakisiwa kuwa na umri kati ya miaka 36 na 40.
Kwa mujibu wa Malengo gari hilo lilikuwa limebakia wafanya biashara na likiwa limesheheni mizigo mbalimbali ikiwemo magunia ya mpunga , mahindi na masanduku ya bia na vinywaji baridi likielekea mjini Mpanda likitokea mnadani kijijini Karema .
Kwa mujibu wa Malengo dereva wa gari hilo ambaye ametambuliwa kuwa Edwin Mgawe (37) mkazi wa mjini Mpanda anatafutwa na Polisi ambapo alifanikiwa kutoroka mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo .
“Uchuguzi wa awali umebainisha kuwa mwendo kasi na uzembe wa dereva ndio hasa chanzo cha ajali hiyo “ alibainisha ,
Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi , Dk Joseph Msemwa amedai kuwa majeruhi wote 32 miongoni mwao wanawake ni kumi na 22 wakiwa wanaume wamelalazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa matibabu .
“Hali za majeruhi zinaendelea vizuri isipokuwa Hans Feso mwenye umri wa miaka 32 hali yake bado ni tete ambapo amekatika miguu yake yote miwili ….Pia miili ya marehemu wawili imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapa” anabainisha Dk Msemwa .
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:
Post a Comment