Home »
» DC MADIWNI WA NSIMBO: TAMBUENI MNAO WAJIBU WA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO KWENYE MAENEO YENU
DC MADIWNI WA NSIMBO: TAMBUENI MNAO WAJIBU WA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO KWENYE MAENEO YENU
Jiunge na Huduma ya Tone Mobile News Bure kabisa kupitia Whatsapp yako na uwe wa kwanza kupata kile kinachotokea ni Rahisi sana Ingia katika uwanja wa kuandika ujumbe mfupi wa maneno katika Whatsapp yako kisha andika TONE MOBILE NEWS tuma kwenye namba 0756364660 utapokea ujumbe kuwa umeunganishwa.
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi Kanali Ngemela Lubinga amewataka Madiwani wa Halmashuri ya Nsimbo kuhakikisha wanatambua kuwa wanao wajibu wa kusimamia miradi yote ya maendeleo ilipo kwenye maeneo yao
Wito huo kwa madiwani aliutowa hapo juzi wakatiakifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Nsimbo uliofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo
Kanali Lubinga alisema Madiwani wamekuwa wakitambua kuwa jukumu la kusimamia miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao sio jukumu lao na badala yake wamekuwa wakiwaachia watendaji wao ndio wasimamie peke yao
Alifafanua miradi mingi imekuwa haiendi vizuri kwenye maeneo yao hivyo wanao wajibu wa kuwasaidia kusimia watendaji wao shuguli za maendeleo zilizopo kwenyw Kata zao na kazi ya Diwani ni kuwasimamia watendaji sio kuwakataa watendaji wao
Alisema Diwani yoyote ambae hatimizi wajibu wa majukumu wala hajuwi wajibu wake huyo sio Diwani na madiwani wa namna hiyo hawanafaida kwa wananchi na kwa Halmashauri
Lubinga aliwaeleza Halmashauri hiyo imebahatika kuwa na rasilimali nyingi ambazo wamekuwa hawazitumii vizuri kwa faida ya Halmashauri ya Nsimba
Alisema yako makampuni yanayochimba madini na makampuni ya wawindaji wa wanyama Halmashauri inapaswa iandae uratibu kwa ajiri ya makampuni haya kabla ya kuanza kufanya shughuli kwenye Halmashauri hiyo lazima makampuni hayo yawe yanachangia kwanza kwenye maswala ya elimu na afya
Alieleza niabu kwa Halmashauri hiyo kuona zipo baadhi ya shule za msingi wako wanafunzi wanasoma huku wakiwa wanakaa chini na badhi ya shule za Sekondari zimeshindwa kukamilisha ujenzi wa majengo ya maabara wakati na makampuni hayo yapo hakikisheni Halmashauri mnaweka utaratibu kwa makampuni kuchangia
Kwaupande wake Mwenekiti wa Halmshauri ya Nsimbo Medi Asenga alisema madiwani watahakikisha maelekezo hayo yaliotolewa watayatekeleza
Alisema Halmashauri hiyo kuanzia saasa itaakikisha shughuli zote za miradi ya maendeleo wanapewa makandarasi wenye uwezo na madiwani wataisimamia miradi hiyo kwa karibu kwa kushilikiana na watendaji wao
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment