Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtoto mmoja aitwaye
Paulina David 3
Mkazi wa Kijiji cha
Sungamila Kata ya Kasokola
Wilaya ya Mlele Mkoa
wa Katavi amefariki Dunia
baada ya kutumbukia ndani ya ndoo ya maji akiwa
nyumbani kwao
Tukio la
kifo cha mtoto huyo lilitokea
hapo juzi Kijijini hapo
majira ya saa kumi jioni wakati
marehemu huyo alipokuwa
nyumbani kwao alipokuwa akicheza
na dada yake
aitwaye Stela David
5
Siku hiyo
mama yake mzazi na
Marehemu huyo aitwaye
Winfrida Sanane alimuacha
nyumbani marehhemu akiwa
anacheza na Dada yake
huyo na yeye alielekea mtoto
kwenda kufua nguo katika mto
ulioko kijijini hapo
Baada ya mama
yao kuondoka marehemu na dada yake
waliendelea na michezo yao
mbalimbali kwa muda mrefu aliambayo ilimsababishia marehemu
apatwe na kiu cha maji ya
kunywa
Ndipo marehemu
alipomweleza dada yake kuwa
anajisikia kiu cha maji na Dada yake alimweleza kuwa kwenye ndoo
ilipo nje karibu na jiko ndio
ina maji ya kunywa hivyo
akanywe maji ya kunywa hapo
Marehemu baada ya kuelekezwa
mahari maji yalipoalielekea hapo na ndipo alipoyaona maji yakiwa yako
kwenye ndoo ya plasitiki yakiwa nusu
ndoo na ndani yake kulikuwa na
babakuli ambalo marehemu
alipoliona alitaka kulichukua kwa ajiri ya kutekea maji ili anywe
Wakati anataka kuchukua bakuli hilo
ndani ya ndoo ya maji ndio alipotumbukia kwenye ndoo hiyo kwa
kutumbukiza kichwa huku miguu ikiwa juu hari ambayo ilimfanya dada yake amkimbilie na kwenda kumtoa ndani ya ndoo
Dada yake
huyo na marehemu baada ya kumtoa mdogo
wake na kumlaza chini alishitushwa ha hari aliyokuwa nayo
na kumfanya akimbie kwenda kwa majirani
kwa ajiri ya kuomba msaada ambapo
majirani walifika kwenye eneo hilo baada ya muda mfupi na kumkuta marehemu
akiwa ameisha fariki Dunia
Kamanda wa Jeshi
la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishana
msaidizi mwandamizi Dhahiri Kidavashari
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
alisema ndugu wa marehemu huyo waliamua kufanya mazishi ya mtoto huyo
hapo jana baada ya kutokuwa na mashaka yoyote kuhusiana
na kifo hicho
0 comments:
Post a Comment