Home » » Mama na mwanae wafa kwa kupigwa na radi wakiwa njiani wakitokea kwa jirani yao‏

Mama na mwanae wafa kwa kupigwa na radi wakiwa njiani wakitokea kwa jirani yao‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Na  Walter Mguluchuma

Mpanda Katavi

Wanawake  wawili  mama  na Mtoto wake wakazi wa Kijiji  cha Mnyagala  Tarafa ya Kabungu Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi wamefariki Dunia baada ya kupigwa na Radi   na Kufa hapo hapo wakati wakiwa njiani  wakiwa wanatokea kwa jirani yao

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa  Mkoa wa Katavi Kamishina mwandamizi Msaidizi  Dhahiri Kidavashari  alisema tukio hilo  lilitokea  hapo  A prili 22 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili jioni kijijini  hapo

Kamanda Kidavashari aliwataja waliokufa kwa kupigwa  na Radi ni Migu  Samwel 46 na mwanae wakike aitwaye Nsungulwa Kasanzu 15 wote wawili wakiwa  wakazi wa kijiji hicho  cha Mnyagala

Alisema kabla ya  vifo hivyo vya mama na mwanae  marehemu hao  walikuwa  wamekwenda kwa jirani yao kwa lengo la kumsalia  na wakati wako huko  waliona wingudogo la  mvua  likiwa  limetanda   hewani

Alieleza kutokana  na  kuwepo  kwa wingu  hilo dogo la  mvua    marehemu  hao walimuga jirani yao  kuwa wanawahi  kurudinyumbani kwao   kabla mvua ya   haija anza  kunyesha  kwani  waliondoka nyumbani  huku  baba mwenye  nyumba  akiwa hayupo  alikuwa amekwenda kwenye shughuli zake za ufundi wa baiskel  kijijini hapo katika eneo linaloitwa  Center

Alifafanua wakati wakiwa wanaelekea  i walipofika jirani  na nyumba yao   umbali wa mita 15  ndipo walipopigwa  na radi  na kufa hapo  hapo   ambapo mama  alipigwa  na radi sehemu  ya kifuani na  mwanae  alipigwa na  radi   sehemu ya kichwani

Alisema baada ya kuwa  wamepigwa na  Radi  na kufafa  hapo hapo  miili ya  marehemu hao iliokotwa  na  majirani  walikuwawakipita  kwenye  eneo hilo baada ya mvua ndogo ilinyesha  kuwa  imekatika

Kidavashari  alieleza  majirani hao   baada ya  hapo walitowa  taarifa kwenye uongozi wa Serikali ya Kijiji  ambao  nao walifika  kwenye  eneo hilo na kisha walitowa taarifa za vifo  vya marehamu  hao kwa jeshi  la polisi  Wilaya  ya Mpanda

Alisema  miili ya  marehemu  hao ilitarajiwa  kuzikwa  jana  kijijni hapo  mara  baada ya  taratibu   za kidaktari  zitakapokuwa  zimekamilika   na  jeshi la Polisi  Mkoa wa Katavi limetowa wito kwa wakazi  wa Mkoa huo huacha kutembea    barabarabi wakati wa mvua  na waepuke  kupita kariu  na miti

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa