Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Katiika
hari isiyoyakawaida Mwendesha Pikiki Bodaboda Mohamed Kalyalya 24
Mkazi wa Mtaa wa Kawajense Madukani Wilayani hapa amejizushia kifo
baada ya kukasirishwa na kitendo cha baba yake kumnyang’anya
pikipiki kwa kumuhofia kupata ajali katika sikukuu ya Pasaka
Tukoio hilo la Bodaboda kujizushia kuwa amefariki Dunia lilitokea
hapo juzi majira ya saa kumi na moja jioni ikiwa ni siku moja baada ya
baba yake mzazi kumnyanga’anya pikipiki ambayo alikuwa amemkabidhi
aitumie kwa shughuli za Bodaboda kitendo ambacho kilimkasirisha
kijana huyo
Siku hiyo ya tukio Mohamed akiwa na rafiki yake aitwaye Kaduga
Antoni ambae wanafanyanae shughuli ya Bodaboda katika eneo la Bar ya
White Club alimshawishi rafiki yake huyo awapigie simu wazazi wake
kwa kutumia simu yake ya mkononi ili awafahamishe kuwa Mohamed
amefariki Dunia baada ya kujiuwa kwa kunywa sumu
Bodaboda huyo mwenzake baada ya kushawishiwa hivo alipiga simu kwa
wazazi wake na Mohamed na kuwapataarifa za kifo cha mtoto wao
alifariki Dunia kwa kunywa sumu akiwa katika maeneo ya vichaka vya
Shanwe mjini hapa na taarifa hiyo aliwapigia Bodaboda wenzake
wanaofanya shughuli kwenye kituo cha Bar ya White Club
Wazazi wa Bodaboda walipopata taarifa hizo walianza kulia na
majirani walifika kwenye eneo hilo la nyumbani kwao na Bodaboda kwa
ajiri ya kuomboleza msiba kwa jirani yao na walianza shughuli za
kuuweka mji huo katika mazingira ya usafi kwa ajiri ya kuweka msiba
Wakati harakati hizo za kuweka msiba zikiwa zinaendelea Bodaboda
wenzake waliamua kwenda kumtafuta mwenzao kwenye eneo ambalo alidaiwa
kuwa amefia kwa kujiuwa kwa kunywa sumu
Bodaboda hao
walifika katika eneo hilo ambalowalikuwa wameambiwa amefia mwenzao
hata hivyo walifanya jiitihada za kumtafuta kichakani na hawakuweza
kufanikiwa kumwona kwenye eneo hilo
Jitihada za kumtafuta ziliendelea ndipo wakati Bodaboda walifika
kwenye eneo la mtaa wa Kigamboni walimwona Mohamed akiwa anatembea
barabarani na walipomsemesha alitaka kuwakimbia na kisha walimsihi
awaeleze sababu iliyomfanya ajizushie kifo
Katika maelezo yake alieleza kuwa rafiki Kaduga Anton ndiye aliye
chukua simu yake ya mkononi na kuwasambazia wazazi wake na
Bodaboda taarifa za kifo chake hicho
Kwa upande wake Kaduga
aliwaeleza kuwa Mohamed alimpatia simu yake na kumweleza awapigie simu
wazazi wake kuwa amekunywa sumu na amefariki Dunia na aliamua kufanya
hivyo kwa kuwa baba yake siku moja kabla ya tukio hilo alimyang’anya
pikipiki kwa kile alimweleza kuwa na wasimasi na mtoto wake kupata
ajali wakati wa sikukuu ya Pasaka kutokana na tabia yake ya ulevi
0 comments:
Post a Comment