Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi DR Rajabu Rutenwe ameziagiza Halmashauri zote za Mkoa wa Katavi kuhakikisha zinaondoo migogoro yote isiyokuwa na sababubaina ya waalimu na viongozi wa Elimu wa Wilaya na baina ya Wakurugenzi na waalimu
Kauli hiyo ya agizo alitowa hapo juzi wakati akifungua kikao cha kazi kilichowashirikisha viongozi wa elimu kutoka Hamashauri zote nne za Mkoa wa Katavi na viongozi wao wa elimu wa mkoa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Inyonga Wilayani Mlele
Dr Rutengwe alisema anawaagiza viongozi wote wa elimu waakikishe wanawatendea haki waalimu wote na kwaharaka wanapokuwa waalimu wamefika kwenye ofisi zao kwa ajiri ya shida mbalimbali
Alisema wapeni haki zao mapema bila kuwazungusha na kama kunasababu inayokwamisha basi wapeni majibu mazuri yanayowatia matumaini kwa waalimu
Alifafanua kuwa sio jambo jema kuwakatisha tamaa waalimu hasa kwa kutowajali wanakwenda ofisini kwao kwa ajiri ya kupata ufumbuzi wa shida zao mbalimbali zinazokuwa zinawakabili
Mkuu wa Mkoa alieleza kuwa yapo malalamiko wanayolalamikiwa viongozi kuwa wamekuwa na tabia ya kutowajali waalimu kwa kuwatolea majibu yasiyoridhisha kuwakashifu na kuwadharau waalimu au kuwaonyesha ukubwa wao kwenye ofisi zao
Hivyo ni vema tabia hiyo waiashe na wajirekebishe kwa kujenga mahusiano mazuri na waalimu wao kwa kuwa washauri wazuri kwa waalimu ili waweze kutumia vizuri fursa zilizopo katika Mkoa wa Katavi ili ziwasaidie kujiimarisha kiuchumi
Alisema kikao hicho cha kazi ni vema kiwasaidie pia kuzingatia wajibu wao wa kuwajengea waalimu uwezo na moyo mzuri wa kufanya kazi kwa kuwaboreshea mazingira yao ya kufanyia kazi ili wawe na moyo katika ufundishaji ambao utapelekea wanafunzi kufaulu vizuri katika mitihani yao
Alieleza ni vizuri viongozi wakajipima katika ngazi zao za mamlaka ili waweze kujiuliza ni kwanini viongozi wengine wanafanya vizuri ili nawao wajifunze kupitia kwao endapo watafanya hivyo maendeleo ya elimu katika Mkoa wa Katavi yataimarika
Aidha aliwataka viongozi wa elimu wa Mkoa huu kuzisimamia kwa ukaribu Halmashauri zao ili mkoa wa Katavi upate matokeo mazuri zaidi ya ufaulu wa mitihani matokeo ya mtihani wa darasa la saba mwaka 2013 Mkoa wa Katavi ulikuwa wa 13 kati ya mikoa 25 ni vema sasa mkoa ukajipanga vizuri ili uweze kushika nafasi ya juu zaidi
Pia alizitaka Halmashauri kuhakiisha zinasimamia kikamilifu ujenzi wa maabara katika shule zao za sekondari kama ambavyo alivyokuwa amewaagiza ili zianze kutumiwa na wanafunzi kwani maabara hizo zilipaswa kukamilika Desemba mwaka jana 2013
Hivyo atahakisha anapita kukagua kwenye Halmashauri zote ili kuona hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa majengo ya maabara kwenye Sekondari zote na sehemu atakapo kuta ujenzi hauja fanyika hata sita kuchukua hatua stahiki kwa wale walioshindwa kutekeleza kwani agizo hilo la ujenzi wa maabara ni la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
0 comments:
Post a Comment