Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Waletr Mguluchuma
Mpanda Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia Eva Tanganyika 72 Mkazi wa Mtaa wa Mpandahotel kwa tuhuma za kumkamata akiwa na Risasi tisa za bunduki aina ya SAR na risasi za Bunduki ya SMG
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi Francis Maro mtuhumiwa huyo alikamatwa na Risasi hizo tisa hapo Februari 24 mwaka huu majira ya saa tatu na nusu usiku akiwa amezihifadhi isivyo halali nyumbani kwake
Alisema Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata taarifa kutoka kwa Raia wema ambao walifikisha taarifa kwa jeshi la Polisi zilizoelea kuwa ndani ya nyumba hiyo ya Eva kuna risasi zimehifadhiwa ndani ya nyumba
Kaimu Kamanda alisema upelelezi wa awali uliofanywa na jeshi la Polisi umebaini kwamba mtu aliyekuwa akimilki Risasi hizo ni mtoto wa Eva Tanganyika aliyeweza kufahamika kwa jina la Agustino Tanganyika
Alisema mtoto huyo wa Eva alitoroka kusiko julikana mara baada ya tukio la kukamatwa kwa mama yake na jeshi hilo linaendelea kumtafuta iliwaweze kumkamata
Kaimu Kamana Maro alieleza kuwa kukamatwa huko kwa Risasi ndani ya nyumba hiyo kunaonyesha upo uwezekano mkubwa kwa mtuhumiwa kuwa anamiliki silaha kinyume cha sheria
Katika tukio jingine jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limemkamata Nenmes Ntinda 40 Mkazi wa Kijiji cha Mtisi kata ya Sitalike Wilaya ya Mlele akiwa na Bhangi kete 475 na mali inayosadikiwa kuwa ya wizi Dawa baridi za binadamu zenye nembo ya MSD
Mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo juzi majira ya saa sita mchana akiwa na vitu hivyo ambavyo alikuwa amevihifadhi ndani ya nyumba yake kijijini hapo
Dawa za binadamu zenye nembo ya MSD alizokamatwa nazo ni zaaina ya Diotrim kopo 4 Asdoxin kopo 2 A strogly kopo 2 Gloves box 1 Coartem box 3 Amoxicilin box2 Co Tzimoxazale box 1 na bomba za sindano box 1 na jumla ya thamani y dawa hizo bado haijafahamika
0 comments:
Post a Comment