Home » » WAUMINI WAKISLAMU WAPIGANA MAKONDE MSIKITINI WAKIMPINGA IMAMU WAO MPYA‏

WAUMINI WAKISLAMU WAPIGANA MAKONDE MSIKITINI WAKIMPINGA IMAMU WAO MPYA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
katika hariambayo haikutarajiwa  waumini wa Dini ya Kislamu wanaosari katika Msikiti wa Mji wa  Zamani  uliopo katika mtaa wa MjiMwema  Wilayani Mpanda  wamepigana  makonde ndani ya Msikiti  kutokana na  na pande mbili kupingana   baini yao juu ya nani awe  Imamu wa Msikiti huo
Tukio hilo  la aina yake liltokea  hapo Februari 21 mwaka huu majira ya  saa nane  mchana mara baada ya kumalizika kwa ibada ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti huo iliyokuwa ikiongozwa  na Shehe  Hussein Mkumba
Hari ya hewa ndani ya msikiti huo ilibadirika  mara baada ya swala hiyo ilipomalizika  ambapo Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Katavi Ally Hussein ambae pia ndiye shehe mkuu wa wilaya ya Mpanda  aliposimama na kuwaeleza waumini hao  kuwa hatua inayofuata ni ya kumkabidhi hati ya Uimamu  mpya wa msikiti huo Yassin Kasote
Baada ya kuuli hiyo Shehe  Ally Hussen alianza kusoma hati hiyo  kitendoambacho kiliwaudhi baadhi ya waumini hao ambao  hawakubaliana  kuongozwa na Imamu Yassin Kasote ambaye alichaguliwa  hivi karibuni katika uchaguzi uliofanyika Januari 29 baada ya kumshinda  mgombea mwenzake wa  nafasi hiyo Muajiri Mzee
Wakati  akiendelea kusoma hati hiyo kundi hilo linalompinga  Kasote  liliokuwa likiongozwa  na Ally Kibauka Mawisa  walikwenda kufunga milango ya misikiti huo na kutangaza kuwa atoki mtu humo ndani
Baada ya kufunga milango walimfuate Kasote  wakimtaka  awapatie  hati ambayo alikuwa amekabidhiwa na viongozi wa Bakwata waliokuwa wameongozwa na Kaimu shehe wa Mkoa wa Katavi  kitendo  ambacho Kasote kakukubaliana nacho
Shehe  Kasote  alipoona anataka kupolwa hati hiyo alianza  kuwashambulia kwa makonde  hari ambayo iliwafanya waumini wanao muunga mkono  nao kuungana nae  hari ambayo ilisababisha mapingano kuanza  baina ya pande hizo mbili
Hata hivyo  wakati mapingano yakiwa yanaendelea  baadhi ya waumini waliokuwa ndani ya msikiti huo wakiwemo askari polisi wa  Dini hiyo waliweza kufanikiwa kufungua milango ya msikiti huo  na kufanikiwa kumaliza vurugu hizo na kisha makundi hayo yote mwawli walikwenda kituo cha polisi cha mpanda mjini kutoa taarifa kuhusiana na vurugu hizo
Kwa upande Kaimu Shehe Mkuu wa Mkoa wa Katavi Shehe  Ally Hussen  amewaomba waumini wa Dini  hiyo ya Kisramu  wawe na utelivu  wakati wa kipindi hiki cha mgogoro huo
Amesema  kikubwa anachotaka waumini wa Dini hiyo  ni kuhakikisha wanaendeleza amani katika msikiti huo sio  kuleta machako  ndani ya msikiti na nje ya msikiti
Nae mmoja wa kundilinalompinga Imamu mpya alisema wao hawakotayari kuongozwa na Imanu Yassin Kassote kutokana na  uchaguzi uliofanyika wa kumchagua ulikiuka taratibu za katiba yao
Jeshi  la polisi Mkoa wa Katavi limekiri kuwepo kwa  vurugu kwenye ibada hiyo siku hiyo ya tukio   katika msikiti huo wa Mji wa Zamani

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa