Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
N a Walter Mguluchuma
Katavi
Mkazi wa kijiji cha Ikola Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Richard Clavery 34 amefikishwa Mahakamani katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda kujituhuma za kufanya vitendo vya ushirikina wa kufukua kaburi la mwanamke alikufa
Mtuhumiwa alifikishwa kizimbani hapo Februari 25 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa na kusomewa mashitaka na mwendesha mashitaka Godfrey Luzabila
Mwendesha mashitaka alidai Mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo hapo Februali 18 mwaka huu majira ya saa nne usiku nyumbani kwa Lenada Sakafu
Mwendesha mashitaka Luzabila aliiambia mahakama kuwa siku hiyo ya tukio mtuhumiwa alifika nyumbani kwa Lenada Sakafu na kufukua maiti ya mdogo wake na Lenada aitwaye Tabu Omera ambae alikuwa amefarii siku tatu kabla ya tukio hili
Aliendelea kuieleza Mahakama siku hiyo Lenanda alikuwa nyumbani kwake pamoja na majirani na ndugu zake wakiendelea kuomboleza msiba ghafla alitokea mtoto wake aitwaye Brandina na kuwaeleza kuwa ameona mtu nje akifukua kaburi la marehemu ambae alikuwa amezikiwa kwenye eneo la nyumba yao
Alieleza ndipo watu hao walipoamua kutoka nje na kumkuta mtuhumiwa Richard Clavery akifukua kaburi hilo huku akiwa amevua nguo zake zote ambazo alikuwa amezitundika kwenye msalaba wa kaburi hilo na walipomsemesha mtuhumiwa alijifanya kupandisha majini
Mtuhumiwa baada ya kusomewamashitaka alikana na Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga Ntengwa aliharisha kesi hiyo hadi hapo machi 6 na mtehumiwa alipelekwa lumande baada ya kushindwa kutimiz mashariti ya mdhamana ambapo alitakiwa adhaminiwe na mtu mmoja kwa dhamana ya shilingi milioni moja
0 comments:
Post a Comment