Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Watu wawili James
Mauto 21 Mkazi wa Kijiji cha
Ugala Wilaya ya Mlele na January
Marekani 18 Mkazi wa Kijiji cha Mtapenda
Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele
mkoa wa Katavi wameuwawa kwa kupigwa
risasi na Askari wa Geme Reserve wakati wakiwa wanavua
samaki ndani ya Hifadhi
ya Pori la akiba la Ugala na mwenzao mmoja kujeruhiwa kwa Risasi sehemu ya mbavu zake
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi
Dhahiri Kidavashari tukio hilolilitokea
hapo Februari 28 mwaka huu majira ya saa tisa Alasiri
ndani ya Hifadhi ya pori la akiba
la Ugala Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi
Alieleza siku
hiyo ya tukio James Mauti na
Januari Marekani walikuwa wakivua samaki ndani ya mto Ugala uliko
kwenye Hifadhi ya pori la akiba la ugala wakiwa na mwenzao
mmoja aitwaye Seif Juma
40 Mkazi wa kijiji cha Mtapenda
Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele
Kamanda
Kidavashari alisema wakati wakiwa
wanaendelea kuvua samaki ndani ya mto huo alitokea Askari wa Geme
Reserve ambae alikuwa amevalia sare huku akiwa na silaha bunduki
ambayo haikuweza kufahamika aina yake
Alisema Askari
huyo aliwaamuru wavuvi hao wajisalimishe kwake hata hivyo wavuvi hao
waliokuwa wakiendelea na uvuvi kufutia amri hiyo ya Askari waliamua
kutupa nyavu zao walizokuwa
wakivulia samaki na kukimbia mbio kila mmoja sehemu yake
Ndipo Askari
huyo alipoanza kuwarushia
risasi wavuvi hao na
kuwauwa kwa risasi James Mauto na Januari
Marekani na kumjeruhi Seif Juma sehemu za mgongoni na kwenye mbavu
Majeruhi ambae ni Seif
Juma alifanikiwa kufika katika kijiji cha Ugala
na kutoa taarifa kijijini hapo
kwa uongozi wa Serikali ya Kijiji juu ya tukio hilo na aliweza kupatiwa msaada wa kukimbizwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa ajiri ya matibabu
Kamanda
Kidashari alieleza kuwa mvuvi huyo ambae ni majeruhi kwa kuhofia kukamatwa na kuhojiwa na polisi
baada ya kufikishwa Hospitali
alitoroka na mpaka sasa haijajulikana mahari alipo na anatibiwa wapi
majeraha yake ya risasi
Alisema kutokana na tukio hilo kuhusishwa na Askari
wa Geme Reserve katika hifadhi hiyo
jeshi la polisi Mkoa wa Katavi
linawasiliana na mkuu wa kikosi cha
wanyama pori mkoa wa Tabora ambako ndio
walikuwa wametoka Akari waliohusika na tukio la mauwaji hayo
Alifafanua kuwa
tayari mkuu wa Kikosi hicho cha
wanyama pori ametuma kikosi chake kwenye
eneo hilo la tukio ilikubaini ni Askari
gani waliokuwa kwenye doria eneo hilo
ili kuwabaini na kisha sheria ichukuwe mkondo wake kwa askari
aliyehusika au waliohusika kwa
tukio la mauwaji hayo ya kinyama kwa binadamu hao
0 comments:
Post a Comment