Home » » WATATU WAKAMATWA KWA WIZI WA PIKIPIKI WALIOIPOLA KWA KUTUMIA SMG‏

WATATU WAKAMATWA KWA WIZI WA PIKIPIKI WALIOIPOLA KWA KUTUMIA SMG‏

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi  linawashikilia watu watatu kwa tuhuma  za  kuwakamata na Pikipiki  moja  aina ya Sunlg  walioipola kwa kutumia silaha  pia watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na Risasi  moja  ya bunduki aina ya  Short gun
Watumiwa  walikamatwa hapo  Septemba 16  mwaka huu majira ya saa moja  usiku  huko katika Kijij cha  Uzega Kata ya Utende  Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  aliwataja watuhumiwa  waliokamatwa  kuwa ni Samwel Augustineo  (36) Rashid  Maulid  (32) na John Munjira (27) wote wakazi wa Kijiji cha Goweko  Wilaya ya Sikonge Mkoa wa Tabora
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari  watumiwa  hao  wanadaiwa siku hiyo ya Septemba 16  majira ya saa nane  mchana  watumiwa  Walimpola  Jirangara  Kabati  50  pikipiki aina ya Sunlg  yenye Namba za usajiri Lbrstjb52 C9004775 wakati  akitoka kijijini kwake Mwamayunga  akielekea Wilayani Sikonge  
Pia katika tukio hilo watuhumiwa walipola pesa tasilimu  shilingi elfu hamsini pamoja na simu moja  aina ya Nokia yenye thamani ya Tsh40,000 mali ya Jirangara Kabati
Alieleza  watuhumiwa  baada ya kupola  pikipiki  hiyo waliondoka  Wilayani Sikonge   na kuelekea  Tarafa ya Inyonga  Wilaya ya Mlele Mkoa wa  Katavi kwa lengon kuiuza
Jeshi la polisi kituo cha Inyonga  walipata taarifa  kutoka jeshi la polisi Wilaya ya Sikonge kuhusiana na watuhumiwa hao  kuwa wa wamekimbilia katika Tarafa ya Inyonga  na ndipo  walipo anza msako  na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na Pikipiki hiyo  pamoja na Risasi moja ya Bunduki ya Shot  Gun
Kamanda wa polisI kidavashari  alieleza kuwa baada ya kuhojiwa  na  polisi  watuhumiwa hao wamekiri  kuwa wamekuwa wakijihusisha kwenye matukio mbalimbali ya unyang’anyi  wa kutumia  silaha  aina ya Shot Gun
Alisema watuhumiwa  wanatarajiwa kusafirishwa hadi Wilayani Sikonge  ambako  ndiko walikofanyia kosa hilo ili waweze kufikishwa Mahakamani  kujibu  mashitaka

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa