Home » » PSPF yatoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 4 kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi aliyosomea Pinda‏

PSPF yatoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 4 kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi aliyosomea Pinda‏

 



Katibu tawal wa mkoa wa Katavi Eng. Emmanuel Kalobelo aliye kwenye kiti akimsikiliza kwa makini meneja mfawidhi wa mfuko wa hifadhi wa PSPF wa mkoa wa Katavi Ileth Mawala wakati akimkabidhi  mchango wa shilingi Milioni nne na laki nne zilizotolewa na PSPF kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Kakuni aliyosomea Waziri Mkuu Pinda iliyoko katika kata ya Kibaoni wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi. msaada huo umekabidhiwa katika ofisi ya Katibu tawala wa mkoa wa katavi aliyepokea msaada huo kwa niaba ya uongozi wa serikali ya mkoa wa katavi
Picha na Walter Mguluchuma


Na  Walter Mguluchuma
Mfuko wa hifadhi ya  jamii  wa (PSPF)  umekabidhi  msaada wa zaidi ya shilingi milioni  nne kwa ajiri ya ukarabati wa  shule ya Msingi Kakuni  aliyosoma  Waziri Mkuu Mizingo Pinda  iliyoko  katika Kata ya Kibaoni Wilaya ya Mlele   Mkoa wa Katavi  ambayo majengo  ya shule hiyo yamechakaa
Msaada huo  ilikabidhiwa hapo jana na  Meneja  Mfawidhi  wa NSPF wa Mkoa wa Katavi  Ileth Mawalla  kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa (PSPF) wa Taifa  katika ofisi ya Ktibu Tawala wa Mkoa wa Katavi
Akipokea hundi hiyo yenye thamani ya shilingi 4,000,000   katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Mwandisi Emanuel  Kalobelo  alisema msaada huo umepokelewa  kufuatia  maombi mbalimbali  yalikuwa yametolewa  na uongozi wa Serikali wa Mkaa wa Katavi  kwa wadau mbalimbali  ambao waliombwa waichangie shule hiyo ambayo majengo yake  yamekuwa machakavu
Alisema  shule hiyo  majengo yake yako katika hari mbaya ya uchakavu  hivyo  Mkoa uliamua  kujenga upya shule hiyo ikiwa kama sehemu ya kumuhenzi  Waziri Mkuu Mizengo Pinda
Kalobelo  alieleza kuwa  ujenzi huo  mpya wa Shule ya Kakuni  mpaka utakapo kamilika utagharimu  jumla ya shingi  Bilioni 4 .4 na tayari  majengo  ya madarasa 14  yanakaribia kukamilika kwa  kupitia misaada ya wafadhili mbalilimbali  wa ndani ya  Nchi na Nje ya Nchi
Majengo mengine ambayo yanatarajiwa kujengwa kwenye shule hiyo ya Kakuni  ni nyumba  kumi na mbili za  waalimu Bwalo la mikutano    ofisi za waalimu na chuma cha kujifunzia kompiyuta kwani shule hiyo inatarajiwa kuwa  ni ya kisasa
Katibu Tawala huyo alisema kuwa lengo la Serikali katika Mkoa wa Katavi  ni kuhakikisha  wanafunzi  wanasoma kwenye mazingira mazuri  katika shule zote zilizopo  katika Mkoa huo si o kwa shule ya Kakuni peke yake
Aidha amewashukuru wadau mbalimbali ambao wameisha anza kuchangia ujenzi wa shule hiyo  na ammetowa wito kwa wadau wengine nao  wajitokeza   kuchangia  shule hiyo na shule nyingine zilizopo katika Mkoa wa Katavi ili kuweza kuboresha  mazingira  ya elimu
Kwa upande wake Meneja wa(PSPF)  wa Mkoa wa Katavi Ileth Mawalla  alisema mfuko huo  umechangia msaada huo kama sehemu ya wadau  wa elimu hapa Nchini
Alisema  (PSPF)  imekuwa ikitowa  misaada mbali mbali   ya maendeleo kwenye maeneo mbalimbali  yanayo wazunguka hasa kwenye maswala ya elimu Afya  na huduma nyingine za kijamii 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa