Home » » BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA AZIMIO LA KUANZISHA KATA MPYA SITA NA MITAA 30 ‏.

BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA AZIMIO LA KUANZISHA KATA MPYA SITA NA MITAA 30 ‏.



 Mwenyekiti wa Hakmashauri ya Mji wa Mpanda Enock Gwambasa akihutubia kikao maalumu cha baraza la Madiwani la Mji wa Mpanda lililokutana juzi katika ukumbi wa chuo kikuu huria cha mkoa wa Katavi kujadili na kupitisha kuongeza kata sita na mitaa 30 ambapo hapo awali Halmashauri ilikuwa na kata tisa na sasa zitakuwa 15.
Picha Na Walater Mguluchuma
 Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda wakiwa kwenye kikao maalumu cha baraza la madiwani kilichofanyika juzi katika ukumbi wa chuo kikuu huria cha mkoa wa Katavi kujadili na kupitisha mapendekezo ya kuongeza kata sita na mitaa 30  ambapo awali Halmashauri hiyo ilikuwa na kata tisa na sasa zitakuwa kumi na tano
Picha Na Walter Mguluchuma 

Na  Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Baraza la Madiwani la Halmashauri  ya Mji wa Mpanda  Mkoa wa Katavi limepitisha azimio la kuanzisha Kata sita Mpya na mitaa thelathini  ili kusogeza huduma za kiutawalakaribu na wananchi
Uamuzi huo wa kuongeza kata hizo ulipitishwa jana na kikao maalumu cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Mpanda kwenye kikao cha Baraza hilo  kilichofanyika kwenye  ukumbi wa chuo Kikuu Huria cha Mkoa wa Katavi kilichopo mjini hapo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Enock Gwambasa  alilieleza Baraza hilo kuwa  viongozi  wa walioko katika Halmashauri  hiyo wamekuwa  wakikabiliwa  na tatizo kubwa la  utendaji wa kazi  kutokana  meoneo  mengi wanayo fanyizia kazi kuwa na maeneo makubwa
Alisema  kuongeza kata hizo na mitaa kutasaidia  pia  kuupanga vizuri mji wa Mpanda  ambao kwa sasa  unapanuka kwa kasi kubwa
Nee  Mkurungezi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Selemani Lukanga alieleza Baraza hilo la Madiwani kuwa endapo  mamlaka husika  zitaidhinisha uanzishwaji  wa Kata hizo  na mitaa  Halmashauri ya Mji wa Mpanda  itakuwa  na Kata 15 toka Kata 9 za sasa Mitaa 47  ambapo iliyopo sasa ni mitaa 17  na vijiji tisa kati vitano vilivyopo
Lukangaza alizitaja  kata sita zilipendekezwa kuongezwa kuwa ni Kata ya Mwangaza,Kazima , Majengo ,Uwanja wa Ndege ,Kivukoni na Kata ya Mwamkuru pia wamepanga kuiomba Halmashauri ya Wilaya ya Mle iwapatie Kata ya Kasolola ambayo iko jirani zaidi na Halmashauri ya mji wa Mpanda kuliko ilivyo  kwa Halmashauri ya Nsimbo Wilaya y a Mlele hata wananchi wa Kata hiyo itakuwa rahisi kupata huduma  wanapo kuwa wanahitaji kuhudumiwa
Alisema pamoja na ongezeko la kata hizo Halmashauri  itakuwa na changamoto   la gharama za ongezeko la uendeshaji kwani mapato ya Halmashauri  ya ndani  kwa sasa hivi ni  Tsh 926,549,000 kwa mwaka 
Lukanga alifafanua kuwa  katika kukabiliana na changamoto hiyo ya Halmashauri  imepanga mkakati wa kubuni  mradi wa viwanja  5000 katika maeneo ya mji  na kufanya tathimini ya  kodi ya majengo
Alitaja mkakati mwingine kuwa ni  kufuatilia kwa karibu ushuru  kwa wafanyabiashara   kutunga sheria ndogo  kwa ajiri ya kusimamia  ukusanyaji wa mapato  na kutoza  leseni  za biashara  ambapo apo awali  Halmashauri ilikuwa haitozi  malipo hayo ya ada ya leseni 

NA BLOGS ZA MIKOA

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa