Na Walter Mguluchuma-Blogs za Mikoa
Mpanda Katavi
Watu kumi wamejeruhiwa na kulazwa katika
Hospital ya Wilaya ya Mpanda baada ya
Roli ana ya Fuso walilo kuwa
wakisafiria kupinduka baada ya kushindwa kupanda mlima
Ajari hiyo ilitokea hapo juzi majira ya saa kumi na mbili asubuhi huko katika
Kijiji cha Kanoge makazi ya Wakimbizi
ya Katumba Wilaya ya Mlele Mkoa
wa Katavi ajari ambayo ililihusisha gari
lenye namba za usajiri T 210BBZ aina ya fuso
lililokuwa likiendeshwa na
Makaliasi Mmanzi (36) mkazi wa
Mtaa wa Makanyagio Mjini Mpanda
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri
Kidavashari
aliwataja majeruhi hao kuwa ni Tano Salumu
(16) Matheo Mswanya (27) waliojeruhiwa miguu Juma Maulidi( 41)
alipata majeraha kichwani Salimu Hamisi (27) alipata maumivu kifuani
Abeiry Silivesto (20)
aliye humia kifuani wote wakazi wa Mtaa wa Makanyagio Mjini Mpanda
Aliwataja
majeruhi wangine kuwa
ni Hussein Mohamed (32)
mkazi wa Mtaa wa Nsemlwa aliumia mguu
Simon Canshuni (38) mkazi wa Mtaa wa Kawajense ambae amevunjika
mguu wa kushoto Frenk Masatu (15) Ibrahimu Mnyaki (45) aliye umia
kiono na miguu wakazi zi wa mtaa wa kawajense
na Mazoe Kasanga (30) mkazi wa
Kijiji cha Kakese wote wakazi wa Wilaya
ya Mpanda Mkoa wa Katavi
Kamanda
Kidavashari alieleza kuwa gari hilo ambalo lilikuwa limebeba watu hao lilikuwa
likitokea Mpanda mjini likielekea katika
kijiji cha Ugalla Wilaya ya Mlele mkoani
hapa
Alisema wakati
gari hilo lilipo fika katika eneo la
mlima wa Kanoge lilishindwa kupanda
mlima na kuanza kurudi nyuma na kisha liligonga gema upande wa kulia wa barabara na kupinduka
Majeruhi hao wote wamelazwa katika Hospital ya Wilaya
ya Mpanda wakipatiwa matibabu na watatu kati yao hari zao ni mbaya
Kamanda Kidavashari amewataka wamiliki wamiliki wa vyombo vya
usafirin kujenga utaratibu wa kufanyia matengenezo vyombo vyao vya usafiri na kuzingatia sheria za usalama barabarani
Alisema dreva wa
gari hilo anashikiliwa na polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote ili aweze kujibu mashitaka
0 comments:
Post a Comment