Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Lile tatizo la uhaba wa maji lililokuwa likiwakabili wakazi wa Mji wa
Mpanda kwa kipindi kirefu sasa limepatiwa ufumbuzi na
halitakuwepo tena kuanzia mwakani mara hapo utakapo kuwa
umekamilika mradi wa chanzo cha maji cha Ikorongo kilichopo katika Makazi
ya wakimbizi ya Katumba
Hayo yamesemwa hapo jana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda
Enock Gwambasa mara baada ya ziara yake ya kukagua
mradi huo wa chanzo cha maji cha Ikorongo
Mradi huo wa maji wa chanzo cha Ikorongo umetokana na msaada uliotolewa na
benki ya dunia ambayo ndio itakayogharamia mradi huo ambao ni mkombozi kwa
wakazi wa Mpanda na vijiji vinavyozunguka mji huo
Alisema mradi huo utakapo kamilika unatarajiwa kugharimu
jumla ya shilingi biloni tatu na milioni miatatu na
utakamilika mwezi june mwakani na utamaliza tatizo kabisa kwa mji wa
Mpanda na vijiji vinavyo zunguka mji huo
Alisema eneo la kujengelea chanzo cha
maji kilichopo Ikolongo kinatajiwa kukamilika katikati ya mwezi huu
chanzo hicho cha maji kinauwezo wa kuzalisha lita milioni mbili na laki mbili
kwa siku
Gwambasa alifafanua kuwa ujenzi wa tanki
la kuhifadhi maji hayo lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni
moja utakamilika mwishoni mwa mwezi huu wa oktoba
Alieleza kuwa mara baada ya shughuli hizo kukamilika itafuata
kazi ya uchimbaji wa wa mitaro na usambazaji wa bomba kutoka kwenye
chanzo hicho cha Ikolongo hadi mjini Mpanda
Kwa upande wake kaimu
Mwandisi wa Maji wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Festo Katanti
alieleza kuwa mji wa Mpanda unawakazi 102,360 hivyo
mradi huo utafanya kuwa na zida ya maji ambayo yanaweza pia
kupelekwa hadi kwenye Tarafa ya Nsimbo wilaya ya Mlele iliyoko
katika Halmashauri ya Nsimbo
Alisema maji ambayo
yatakuwa yamezidi kwenye tanki lililopo katika Mtaa wa Kazima
watahakikisha maji hayo hayapotei bure bali wanaangalia utaratibu
wa jinsi yatakavyo tumiwa na wananchi wa jirani na Tanki hilo
Kaimu mhandisi wa maji wa
Halmashauri ya mji wa Mpanda bwana Katanti alieleza kuwa mradi huo wa ujenzi wa
chanzo cha maji na tenki la maji unafanywa na kampuni iitwayo Pet Cooperation
Ltd inayomilikiwa na mkandarasi wa kitanzania
0 comments:
Post a Comment