Home » » MWANAMKE AFA KWA KUGONGWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA BARABARA AKIWA KWENYE KIBANDA CHAKE CHA KUUZA MBOGA ZA MAJANI‏

MWANAMKE AFA KWA KUGONGWA NA MTAMBO WA KUTENGENEZEA BARABARA AKIWA KWENYE KIBANDA CHAKE CHA KUUZA MBOGA ZA MAJANI‏

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja aliye fahamika  kwa jina la  Mariamu  Charles (25) mkazi wa Kijiji cha Mwamkuru  Wilaya ya Mpanda  amekufa hapo hapo  baada ya kugongwa  na mtambo wa  kushindilia barabara  wakati akiwa kwenye kibanda chake cha biashara   ya kuuza mboga za majani  Kijijini hapo
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari tukio hilo lilitokea hapo Septemba 17 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili na nusu jioni katika barabara ya Kotoka kijiji  cha Kakese  kuelekea  Kijiji cha Mwamkuru
Alisema siku hiyo marehemu  alikuwa  kwenye kibanda chake  kilichopo kando ya barabara akiendelea na  shughuli yake ya biashara ya kuuza mboga za majani  kama ilivyo kuwa kawaida yake ya kila siku
Wakati akiwa aiendelea  kufanya shughuli  zake za kuuza mboga za majani  ndipo alipo gongwa na mtambo wa kushindilia barabara  ambao ulikuwa ukiendeshwa na Ally Abdi (31) mkazi wa Mpalamawe Wilaya ya Nkasi na kufa hapo hapo
Kamanda Kidavashari  alieleza kuwa chanzo cha ajari hiyo kilitokana na wafugaji  waliokuwa wakiswaga Ng,ombe zao kandokando ya barabara  ya Mwamkuru  iliyo kuwa akifanyiwa matengenezo na mtuhumiwa  Ally Abdi Ng’ombe hao walionekana  wakifanya uharibifu katika barabara hiyo  kutokana na kukosekana kwa uangalifu mzuri toka kwa wachungaji hao
Alisema kitendo hicho kilimkasirisha mtuhumiwa mwendesha mtambo huyo aliye chukuwa jukumu la kufukuza mifugo hiyo kwa kutumia mtambo aliokuwa akiendesha ndipo alipo shindwa kuhimili mtambo huo wakati akikata kona  na kumgonga marehemu  akiwa kwenye kibanda chake na kufa hapo hapo
Kidavashari alieleza kuwa  uchunguzi wa awali kuhusiana na ajari hiyo umebaini kuwa chanzo cha ajari hiyo ni uzembe wa Drevawa kuendesha chombo  akiwa  amelewa pombe  hari ambayo ilimfanya kutokuwa makini  wakati akiendesha mtambo huo
Alieleza mtuhumiwa alikamatwa  siku hiyo hiyo ya tukio  na atafikishwa Mahakamani  baada ya uchunguzi kukamilika ili aweze kujibu  mashitaka yatakayo mkabili

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa