Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Philbert Silali (19) Mkazi wa Mtaa wa Kazima Mjini
Mpanda anashikiliwa na jeshi la
polisi kwa tuhuma za kumshambulia kwa
ngumi na mateke msichana aliye mkataa kufanya nae mapenzi
Tukio hilo la
wivu wa kimapenzi lilitokea hapo
Septemba 17 mwaka huu majira ya saa saa kumi na mbili jioni katika Mtaa wa Kazima Mjini Mpanda Mkoa wa Katavi
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
alisema siku hiyo ya tukio mtuhumiwa alikutana na Mary Pius (15) na kisha
mtuhumiwa limuomba msichana huyo
awe rafiki yake wa kimapenzi
Alieleza pamoja mtuhumiwa kutowa ombi hilo la kutaka
urafiki wa Kimapenzi kwa msichana
huyo alimkatalilia katakata kwa kile
alicho kieleza kuwa haitaji kuwa na
mausiano ya aina yoyote na mwanaume ya kimapenzi kwa sasa
Baada ya msichana
kumkatalia mtuhumiwa alipandwa na
hasira na ndipo alipoamua kumshambulia
kwa kumpiga ngumi na mateke katika sehemu mbalimbali za mwili wake
Alisema Kamanda
Kidavashari baada ya kuona kipigo kinazidi
msichana huyo alianza kupiga mayowe ya kuomba msaada ambapo aliweza kuokolewa na watu
waliokuwa jirani na eneo hilo
Mtuhumiwa aliweza kukamatwa na watu hao walio
mwokoa msichana aliyekuwa akipata kichato na waliweza kumfikisha kwenye kituo cha
polisi cha Mpanda mjini
Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Katavi alisema mtuhumiwa
anatarajiwa kifikishwa mahakamani baada
ya upelelezi utakapo kuwa umekamilika
0 comments:
Post a Comment