Na Walter Mguluchuma
Serikali ya wilaya ya Mpanda imetangaza kuwahamisha wananchi
wote wanaoishi katika Kitongoji cha Kamama Kata ya Mpandandogo na
kukifunga kijiji cha bugwe kilichopo katika Tarafa ya Kabungu wilayani
hapa kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira.
Uharibifu huo unaofanywa na wafugaji na shughuli za
kilimo na kusababisha uharibifu mkubwa wa msitu wa katuma ambao ndio
chanzo kikuu cha mito mingi katika ukanda wa ziwa Tanganyika
Kauli hiyo imetolewa hapo juzi na mkuu wa wilaya ya Mpanda Paza
Mwamlima wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
Mwamlima alisema zoezi hilo la kuwahamisha watu waliovamia mistu hiyo limeanza hapo septemba 14 na litadumu
kwa muda wa siku kumi na nne na
linawashirikisha Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya, watumishi kutoka ofisi ya Ardhi na Maliasili pamoja
na Viongozi wa Vijiji husika.
Alifafanua kuwa uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mpanda
umeamua kuwahamisha
wananchi wa Kitongoji Kamama kutokana watu hao kuvamia msitu unaotenganisha Kata
ya Mpanda Ndogo na makazi
ya wakimbizi ya Mishamo eneo ambalo lilikuwa limetengwa kwa ajiri ya shughuli
za uwekezaji
Alisema eneo hilo lenye jumla ya hekari 46,000 pia lilikuwa
limetengwa kwa ajiri ya ujenzi wa kambi ya jeshi la kujenga Taifa na
Shughuli za kilimo kwa vikundi vya vijana
Alieleza kuwa zoezi hilo la kuwahamisha watu hao litafanyika kwa kuwaelimisha kwanza
wananchi hao ili waweze kutambua umuhimu wa misitu na tayari eneo la
kuwahamishia limeisha andaliwa katika kijiji cha jirani kinanacha
itwa Vikonge katika kata ya Mpanda Ndogo
Kwa upande wa Kijii cha Bugwe Mwamlima alisema uongozi wa
Wilaya unawasiliana na ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili iweze kutowa
kibali cha kukifunga kijiji hicho kwani Wizara hiyo ndio yenye mamlaka ya
kukifunga au Kukifunga Vijiji hapa Nchini
Alifafanua kuwa kKjiji hicho ndicho kinachozungukwa na msitu
ambao ndio chanzo cha mito
yote muhimu iliyoko katika
ukanda wa Ziwa Tanganyika ambapo
mito mingi imeanza kukauka kutokana na shughuli zinazofanywa za kibinadamu
Uharibifu huo wa msitu wa Bugwe tayari umeisha anza kuathiri wanyama
katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi kutokana
na kukauka kwa mto Katuma unao peleka maii katika mto wa Sitalike ulioko katika
hifadhi ya Katavi kukauka na kusababisha vifo vya Mamba na Viboko ambapo chanzo cha mto huo ni msitu wa
Bugwe
Alisema kutokana na hari hiyo uongozo wa Wilaya umeamua kuinusuru
hari hiyo na kuanzia sasa maeneo yote ya
Hifadhi ya misitu yatawekewa mabango yanayo kataza watu kufanya shughuli za
kibinadamu katika misitu
0 comments:
Post a Comment