Home » » TRA TAIFA YALALAMIKIWA KWA KUSABABISHA KODI KUBWA YA WAFANYABIASHARA MKOA WA KATAV‏I

TRA TAIFA YALALAMIKIWA KWA KUSABABISHA KODI KUBWA YA WAFANYABIASHARA MKOA WA KATAV‏I

N a Walter Mguluchuma
Mpanda
Mamlaka ya Mapato  Taifa (TRA)  imelalamikiwa na wafanya biashara wa Mkoa wa Katavi kuwa ndio chanzo cha wafanyabiashara wa Mkoa huu kutozwa kodi kubwa  tofauti na kipato chao
Malalamiko hayo yalitolewa hapo juzi kwenye mkutano wa wafanya biashara wa Viwanda  wafugaji  na wakulima( TCCRS) uliofanyika juzi kwenye ukumbi wa Super City mjini hapa
Wakichangia hoja kwenye mkutano huo ulioongozwa na mwenyekiti wao wa( TCCRS)  wa Mkoa wa Katavi Hassanal Dalla  wafanya biashara hao walidai kuwa   mamlaka ya Mapato katika Mkoa huu imekuwa ikiwatoza kodi kubwa kutokana na shinikizo linalo toka makao makuu ya Mamlaka hiyo
Mmoja wa wafanya biashara hao Amani Mahera alidai kuwa  Mamlaka hiyo katika mkoa huu imekwa  ikiwakadiria  kulipa mapato bila kuangalia  mzunguko wa pesa  wanazopata  wafanyabiashara wa Mkoa huu
Alisema  Mamlaka hiyo ya Mapato imekuwa ikipangiwa  malengo  ya kukusanya  mapato  na mamlaka ya  TRA  Taifa bila kujua hari halisi ya kipato cha wafanya biashara  wa Mkoa huu
Nae  Gerad  Edward  alisema kodo wanayo lipa wafanya biashara hasa wa dogo  hakilingani  na kipato chao  alitowa mfano  mtu mwenye kibanda cha duka chenye thamani ya shilingi 700,000 amekuwa akilipa mapato ya shilingi 219,000 kwa mwaka  ushuru wa Halmashari kwa ajiri ya kibanda 120,000 na leseni 100,000
Kwa upande wake Afisa ushirika wa Mkoa wa Katavi  Luhiguza  Sesemkwa  ambae alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwenye mkutano  huo alisema  kuwa kumekuwepo na tatizo  la wafanya biashara kulipa kodi kubwa  kutokana na Mkoa kupangiwa malengo ya kukusanya mapato hivyo ina walazimu mkoa husika  kufikia malengo wanayo kuwa wamepangiwa
Alisema    malalamiko hayo  ameyapokea na atayapeleka kwa  viongozi wa  husika ili waone namna ya kutatua tatizo hili
Aidha mwenyekiti wa TCCRS  wa Mkoa wa Katavi Hassanal Dalla aliwahakikishia wafanya biashara hao kuwa kikao kijacho  atahakikisha  kunakuwepo kiongozi anae toka kwenye mamlaka hiyo ya Mapato ili aweze kujibu hoja hizo
Pia aliwataka  wanachama wa TCCRS  watambue kuwa umoja huo ulioanzishwa hizi karibuni Mkoani Katavi ni wa nikwao   na wala sio wa viongozi peke yao

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa