Na Walte
Mguluchuma
Mpanda
Dreva wa shirika
la Kimataifa linalo wahudumia wakimbizi ( UNHCR) katika
Mkoa wa Katavi Amani Malilo
amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela
baada ya kupatikana na hatia ya kuishi na msichana mwenye umri wa miaka 16 Mwanafunzi wa Kidato cha pili
katika shule ya Sekondari ya Mishamo ya Mishamo ilioko katika Makazi ya
Wakimbizi Mishamo Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi
Hukumu hiyo ilitolewa hapo juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahama ya Wilaya Chiganga
Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na pande
zote mbili za mashitaka na utetezi
Awali katika kesi
hiyo mwendesha mashitaka Mkaguzi
msaidizi wa Polisi Razalo Masembo alileza Mahamani hapo kuwa mshitakiwa
alitenda kosa hilo Novemba 27 na Desemba
25 mwaka jana wa 2012
Mwendesha mashitaka alidai kuwa mshitakiwa
Amani ambae ni Dreva Gari aina ya roli mali ya Shirika la kimataifa
linalo wahudumia Wakimbizi (UNHCR)
wa Burundi
katika tarehe hizo
alimtorosha Msichana 16
Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari ya Mishamo ilioko
katika Makazi ya Wakimbizi ya Mishamo
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi nakuishi
nae bila ridhaa ya Wazazi wake
Mshitakiwa alidaiwa kuwa baada ya kumtorosha Msichana
huyo alisafiri nae hadi Wilayani Kasulu
Mkoani Kigoma akiwa na baadhi ya
warumishi wenzake wa shirika hilo linalo
wahudumia Wakimbizi wa Burundi ambapo waliweza kukaa na msichana huyo Kasulu kwa muda wa siku mbili
Ilielezwa
Mahakamani hapo mshitakiwa baada ya
kutoka Kasulu kwa usafiri wa gari la shirika hilo alipia
na Gari hadi ofisini kwake Katika Mtaa wa Mji Mwema na walipo fika
gatini walinzi walihoji juu ya
uwepo kwenye Gari kwa Msichana huyo hata
hivyo mshitakiwa Amani aliwajibu walinzi
kuwa msichana huyo ni mtoto wake
Masembo aliendelea kuimbia Mahakama baada ya kutoka
hapo walielekea kwenye nyumba ambayo alikuwa amepanga mshitakiwa iliko katika
mtaa wa Mji Mwema ambapo walipofika alimwonyesha chumba cha kulala
msichana huyo hata hivyo ilipo fikia mida ya usiku mshitakiwa
aliingia ndani ya chumba cha
msichana huyo na kumtaka wafanye tendo la ndoa hata hivyo mshitakiwa aliambiwa
na msichana kuwa kwa siku hiyo haita wezekana kwani yuko kwenye siku zake
Siku iliyofuata
mshitakiwa alimwachia msichana huyo pesa shilingi elfu tano kwa ajiri ya
chakula kwenye mgawaha wa jirani na walipo
kuwa wakiishi na alimwonya kuwa jirani yoyote atakae muulizia kuwa yeye ni
nani awaeleze kuwa yeye nimwanaye na
Amani na siwe anamwamkia mshikamoo bali awe anamsalimu kwa salamu
yadini ya Kiisramu isemayo Asalamuwaleko
Mshitakiwa inadaiwa waliendelea kuishi na kulala
pamoja na msichana huyo kwa kipindi
chote hicho wazazi wa Binti huyo wakiwa
wanaendelea kumtafuta hadi hapo Machi 2 6 mwaka huu wa 2013 ambapo mshitakiwa
siku hiyo alisahau simu ndipo msichana
huyo alipo mpigia simu mama yake mdogo
Aitwaye Chausiku Adamu anaishi Mtaa wa Kawajense mjini hapa na
alimweleza mahari anapo ishi na mshitakiwa
na siku hiyo hiyo mama yake mdogo alifanya mawasiliano na wazazi wa
msichana huyo wanao ishi katika Kijiji cha Ifumbula makazi ya Wakimbizi mishamo
.
Baada ya wazazi
kufikishiwa taarifa hizo wazazi hao
walilazimika kwenda kituo cha
polisi cha Mpanda mjini na siku hiyo hiyo ya tarehe 26 machi mwaka
huu
mnamo majira ya saa tisa usiku polisi walifika nyumbani kwa
mshitakiwa katika mtaa wa Mji Mwema mjini hapa na kumkuta mwanafunzi
huyo akiwa ndani ya nyumba aliyo kuwa akiishi nae mashitakiwa Amani
Mshitakakiwa
katika utetezi wake mahakani hapo
aliiomba mahakama imwachie
huru kwani ilikuwa ni mara yake ya
kwanza kutenda kosa hili na anafamilia
ya Mke anae ishi Wilayani Kasulu pamoja
na watoto wanamtegemea yeye
Maombi ambayo
yalipingwa vikari na na mwendesha mashitaka
kwa kile alidai kuwa utetezi
huo haumfanyi mshitakiwa aishawishi
Mahakama imwone hana hatia
Hakimu Mkazi
Mfawidhi Chiganga Ntengwa aliiambia
Mahakama kuwa baada ya kuskiliza
mwenendo mzima wa kesi hii Mahakama
imelidhika na ushahidi ulio tolewa Makamani hapokwa upande wa mashitaka na
utetezi
Hivyo mshitakiwa
Amani amepatikana na hatia ya
kuvunja sheri Namba 134
kifungu namba 16 cha kanuni ya
adhabu cha mwaka 2002 na
kifungu namba 130 (1) (2) (e) na
131 (1)
(3) sura ya 16 cha mwaka 2002 ambapo
mshitakiwa anatakiwa kulipa faini
ya shilingi laki moja au kwenda jela miezi sita hata hivyo mshitakiwa aliweza
kulipa faini hiyo
0 comments:
Post a Comment