Home » » Bodaboda jela miaka saba kwa wizi wa pikipiki‏

Bodaboda jela miaka saba kwa wizi wa pikipiki‏

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mahakama ya Hakimu  Mkazi ya Wilaya ya Mpanda imemuhukumu mwendesha pikipiki  Bodaboda Robarti  John( 25)  mkazi wa Mtaa wa Mkazi wa Mtaa wa Kawajense Wilaya ya Mpanda kifungo cha miaka saba jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa kuiba pikipiki
Hukumu hiyo ilitolewa hapo Septemba  5 mwaka huu wa 2013 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda  Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa  Mahamani hapo  wa upande wa mashitaka na utetezi
Awali katika kesi hiyo mwendesha mashitaka Mkaguzi msaidizi wa Polisi Razalo Masembo  aliieleza  mahakama kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo  hapo Februari 14   mwaka huu majira ya saa moja   asubuhi  katika eneo la Soko la Buzogwe  Mjini Mpanda
Mshitakiwa alidaiwa  siku hiyo ya tukio  aliiba bikipiki   aina ya Sunlg  yenye namba za usajiri  T,534 CCE  yenye thamani ya shilingi milioni moja na raki saba mali ya  Adelahaida Thomas
Mwendesha mashitaka  Masembo  alieleza   mshitakiwa baada ya kuiba pikipiki hiyo  alikwenda nayo hadi katika  Makazi ya Wakimbizi ya Katumba kwa lengo la kwenda kuiuza  hata hivyo hakufanikiwa kumpata mteja wakununua
Mshitakiwa baada ya kukosa  mteja katika makazi ya Wakimbizi ya Katumba Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi aliamua kuondoka na pikipiki hiyo ya Wizi hadi Mkoani Tabora
Masembo aliendelea kuieleza Mahakama  baada ya kufika Tabora  jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi lilipata taarifa  kuwa mshitakiwa amekimbilia mkoani Tabora na ndipo walifanya mawasiliana na polisi wa Mkoa wa Tabora  ambao walifanikiwa kumkamata mshitakiwa akiwa na pikipiki  ya wizi  na kisha walimsafirisha hadi Wilayani Mpanda
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Chiganga  Ntengwa  alieleza kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa Mahakamani  mahakamani  imemwona mshitakiwa ana hatia ya wizi wa pikipiki
Hivyo kutokana na kifungu cha sheria namba  265 sura ya 16   cha mwaka 2002 mahakama imemuhukumu Mshitakiwa Robart john Kifungo cha mika saba jela  ili iwefundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa