Home » » NDUGU WAGOMBEA MAITI MOCHWARI WAWEKA MISIBA MIWILI TOFAUTI‏

NDUGU WAGOMBEA MAITI MOCHWARI WAWEKA MISIBA MIWILI TOFAUTI‏

N a  Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Katika hari isiyo  ya kawaida  ndugu wa Marehemu  wamejikuta  wakigombea  maiti ya Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Itenka(B)  Tarafa ya Nsimbo  Wilaya ya Mlele  Mkoa wa Katavi Philipo Sigareti (32) na kusabishamsiba kuwekwa sehamu mbili  tofauti  
Tukio hili ambalo limevutia hisia za mbalimbali za Wananchi wa Mji wa Mpanda  limetokea  hapo  jana  katika  katika chumba cha kuhifadhi maiti katika  Hospital ya Wilaya ya Mpanda
Marehemu Philipo  alifariki   Septembe  9  mwaka huu   majira ya saa tano na   ya saa sita mchana  katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kutokana na ugonjwa wa moyo  baada ya marehemu kufariki  wanandugu  walishauriana  na kukubaliana kutomzika Marehemu mpaka hapo kaka mkubwa wa Marehemu  aitwaye  Mathias Sigareti  atakapo kuwa amefika kutokea  Kijiji cha Kasanga Wilayani Nkasi Mkoa wa Rukwa alikuwa akifanya kazi ya kufundisha shule ya Msingi
Baada ya  maamuzi hayo kulizuka mgogoro baina ya pande mbili za  ndugu  ambapo  kil Thobias Kazimzuri  alichukua jukumu la kuweka msiba nyumbani kwake Katika Mtaa wa Makanyagio  kwa kile alicho dai kuwa yeye ndio aliye kuwa akimuhudumia marehemu wakati  mgonjwa   huku dada yake  na Thobias  aitwaye Magret Fransis  nae  akipinga kitendo vha kaka yake kuewka msiba kwake Makanyagio  hivyo na yeye kuamua kuweka msiba nyumbani kwake katika mtaa wa Majengo 
Kaka mkubwa  wa Marehe   aliwasiri  hapo  usuku wa kuamkia jana  na kuamuru maerhemu  azikwe jana na msiba uwe nyumbani kwa Magreti  Katika mtaa wa Majengo na sio kwa Kazimzuri  katika  mtaa wa Makanyagio  uamuzi ambao ulipingwa na baadhi ya wanandugu akiwemo na mke wa marehemu  msiba kuwekwa   kwa dada wa marehemu
 Wanandugu wa Pande mbili hizo kila upande uliendelea na taratibu  za kufanya mazishi  na kuanda  kaburi  katika   maeneo tofauti  katika makaburi ya  Mwangaza  yalioko mjini Mpanda
Baada ya kumaliza maandalizi ya kuandaa kaburi pande hizo mbili kila  moja ilielekea katika  chumba cha kuhifadhi maiti  kwa lengo la kuuchukuwNDUGU WAGOMBEA MAITI MOCHWARI WAWEKA MISIBA MIWILI TOFAUTIa mwili wa marehemu  hata hivyo  walianza kutupiana  meneno ya kashifa  kuwa  upande wa Kazimzuri  unataka kuchukua msiba ili kula pesa za rambirambi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi dhahiri Kidavashari ambae  nae  alikuwa amewasiri  kwenye eneo hilo huku akiwa na kundi la askari  ilimlazimu  aingilie  kati kunusuru  hari ya vurugu katika chumba hicho cha kuhifadhi maiti
Kamanda huyo wa polisi aliwaomba wanafamilia hao kama watashindwa kuelwwana basi waende mahakamani  ambapo Mahakama itatowa uamuzi  juu ya mgogoro huu

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa