Na Walter
Mguluchuma
Mpanda
Viongozi wa
Serikali wa Wilaya ya Mpanda wameagizwa
kuwachukulia hatua watu wote waliohusika
na ubadirifu wa miradi mbambali ya ujenzi wa majengo na barabara zikiwemo pesa
shilingi milioni 75 za ujenzi wa madarasa mawili yashule ya Msingi
Azimio ya walemavu wa mtindio w aubongo
katibu wa Idara
ya ikikadi na uenezi wa CCM Wilaya ya Mpanda Joseph Lwamba alisema maagizo hayo yametolewa hapo jana
katika kikao cha kamati ya siasa ya Wilaya ya Mpanda
Alisema katika
kikao hicho cha kamati ya siasa ya Wilaya hii
kimebaini uwepo wa ubadilifu wa fedha katika idara ya ujenzi na idara ya Ardhi inalalamikiwa na wananchi
kutokana na kero mbalimbali hivyo
wamemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mpanda na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
Mji huu kuwachukulia hatua wale wote waliohusika na ubadilifu huo
Lwamba aliitaja
miradi ambayo imefanyiwa ubadirifu ni
ujenzi wa madarasa mawili kwaajiri ya
wanafunzi wenye mtindio wa ubongo katika shule ya Msingi Azimio iliyopo katika
Halmashauri ya Mji wa Mpanda ambapo Serikali ilitowa shilingi milioni 50 hapo mwaka 2010 na Halmashauri ikatowa
milioni 25 na kufanya jumla ya shilingi milioni 75
Alifafanua kuwa
pamoja na fedha hizo majengo ya madarasa hayo mawili mpaka sasa hivi hayaja
kamilika
Aliitaja miradi
mingine inayo daiwa kuwa na ubadirifu wa
fedha ni majengo mawili ya Maabara
Katika shule ya Sekondari ya Misunkumilo
ambayo kamati ya Siasa ilipo ya tembelea ikiwa wataalumu mbalimbali walibaini kuwa majengo
hayo yamejengwa chini ya kiwango na kiasi cha pesa shilingi milioni 17
hazijulikani zilikwenda wapi
Katibu huyo wa uenezi alieleza
miradi mingine ni ya ujenzi wa Barabara katika eneo la Mtaa wa Air Tel
ambapo kamati hiyo
imemwagiza mkuu wa Wilaya awasilshe kwenye kikao kijacho taarifa
inayoonyesha kiasi cha pesa zilizotumika kwenye ujenzi wa barabara hizo
Pia walimuagiza
Mkuu wa Wilaya hii na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji kutowa taarifa kwenye kikao kijacho juu ya
ujenzi wa barabara ya Kakese Mwamkuru ambayo imejengwa chini ya kiwango na kamati hiyo imehoji kwanini mkandarasi
alikuwa anapeleka vifaa usiku na kufanya kazi usiku ndioinaweza ikawa chanzo cha barabara hiyo
kujengwa chini ya kiwango
Kwa upande wa
Idara ya Ardhi kamati ya siasa ya Wilaya ya Mpanda imemwagiza mkuu wa
Wilaya huhakikisha idara ya Ardhi
inawapatia kiwanja cha ekari 20 kanisa la KKKT chenye namba 1417FF ambacho
walikiomba tuka mwaka 2007 na walilipia shilingi 1,137,000 mpaka sasa bado
wanazungushwa kupewa hivyo kamati hiyo
imemwagiza afatilie na wapewe kwa bei ile le ya wakati ule
Nae mwenyekiti wa
Halmashari ya Mji wa Mpanda Enock Gwambasa
alisema ni kweli Halmashari ya
Mji wa Mpanda inakabiliwa na changamoto hizo
zilizo tolewa na kamati ya siasa
ya Wilaya hii
Alisema tayari Halmashari yake imeisha anza kushughulikia changamo hizo
na kwa kuwachukulia hatatua
mbalimbali baadhi ya watumishi waliohusika na
wakandarasi kurudia kazi kwa
gharama zao
Kwa upande wake
mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima
alisema kuwa yeye ni mjumbe wa
kamati ya siasa na hakuwepo kwenye kikao
hicho na wala alikuwa haja
fikishiwa matamko hayo kwa maandishi
zaidi ya kuulizwa taarifa hizi
kupitia mwandishi wa habari hizi
Kwa mujibu wa
vyanzo vya habari inadaiwa mkuu hiyo wa
Wilaya aliitwa kwenye kikao hicho lakini
hakuweza kufika kwa kile alicho dai kuwa ana wageni
0 comments:
Post a Comment