Walter
Mguluchuma-Mpanda.
IDARA ya ardhi katika Halmshauri ya Mji wa Mpanda mkoani Katavi inashutumiwa kwa kushindwa kuwapatia wakazi wa mji huo hati za viwanja kwa miaka kadhaa sasa hivyo kusababisha wakazi hao kuendelea kuwa maskini ..
Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mpanda, Beda Katani wakati akichangia katika mkutano wa wadau uliokuwa ukijadili Mpango Kamambe wa Mji wa Mpanda uliofanyika juzi mjini hapa .
Mpango huo Kamabe wa Mji wa Mpanda unatoa dira ya ukuaji wa
mji huo ambao unaandaliwa kuwa Manisipaa tarajiwa mika kumi ijayo ikiwa ni jitihada za makusudi za kukabiliana na tatizo sugu la bomoa bomoa za mara kwa mara kutokana na makazi wa watu katika miji kujengwa kiholela .
Bila ya kuumauma maneno alisema kuwa kutokana na uzembe huo wa maofisa wa idara hiyo ya ardhi ume sababisha kero kubwa na umaskini kwa wakazi wengi wa mji huo kwani wanashindwa kukopa katika taasisi za kibenki kwa kuwa hawana hati za viwanja wanavyomiliki kihalali .
“Wakazi wa mji huu sasa wanaendelea kuwa maskini kutokana na maofisa ardhi kushindwa kuwapatia hati za viwanja wanavyovimiliki kihalali hii inasikitisha sana kwani baadhi ya wanamiliki na kujenga nyumba zao kwenye viwanja hivyo bila kuwa na
hati hiyo kwa zaidi ya mika hadi kumi “ alisema .
Hoja hiyo iliungwa mkono na wadau wengi mkutanoni humo huku wakiitaka Idara ya Ardhi katika Halmshauri hiyo ya Mji Mpanda kuharakisha upimaji wa viwanja ili kuepusha ujenzi holela wa makazi ya watu unaoendela kwa kasi kubwa katika viunga vya mji huo .
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpanda Mji , Selemani Lukanga alisema kuwa Mpango huo Kamambe wa Mpanda Mji ulioanza 2010 unao tarajiwa
kumamilika 2034
utarahisisha mji huo kutekeleza kwa vitendo sheria ya
ardhi ya namba 4 ya mwaka 1999.
Sheria ambazo zinahimiza upangaji
,usimamiaji na utekelezaji wa mipango kabambe ya matumizi ya ardhi ili
kudhibiti na kuratibu ukuaji wa miji na kuufanya mji
kukua katika mpangilio uliokusudiwa
Aliongeza kuwa pamoja
na mafanikio hayo bado Halmshauri hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo ongezeko la watu na shughuli za kiuchumi
,uelewa mdogo wa wananchi juu ya sheria na taratibu za
uendelezaji wa mji .
“Ujenzi holela wa
makazi ya watu , uhaba mkubwa wa wataalamu pamoja na ongezeko la shughuli zisizo rasimi na
ufinyu wa bajeti katika kutekeleza mpango huu ni changamoto kubwa tunazo kabiliana nazo kwa sasa “ alisisitiza
huu unatowa
dira ya ukuaji wa Mji wa Mpanda ili kuandaa Manisipaa
tarajiwa ya Mpanda na kuondoa tatizo la mji kutokuwa kwenye mpango
maalumu kama ambavyoilivyo kwenye baadhi ya miji ambayo haiko
kimpangilio na matokeo yake kumekuwa na bomoa bomoa za mara kwa mara
0 comments:
Post a Comment