Na Walter
Mguluchuma
Mpanda
Watu wawili
wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoa wa Katavi
kwa tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya aina Bangi gunia tatu za
Bangi na mbegu zake kilo mbili zikiwa
zimehifadhiwa nyumbani kwa watuhumiwa
Kamanda wa jeshi
la polisi Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
aliwataja waliokamatwa na kushikiliwa na jeshi hilo kuwa ni Lungula Pina(
35) na Agustino Pascal( 60) wote wakazi
wa Kijiji cha Kapanga Tarafa ya Mwese Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi
Alisema
watuhumiwa walikamatwa kijijini hapo mnamo Agosti 1 mwaka huu majira
ya saa tisa na nusu alasiri wakiwa
na madawa hayo ya kulevya aina ya
Bangi gunia tatu na mbegu zake kilo mbili
Kidavashari
alieleza watuhumiwa walikamatwa kufuatia taarifa za
zilizokuwa zimelifikia jeshi la polisi kuwa watuhumiwa hao wanajishughulisha na biashara ya kuuza na kusambaza Bangi na kulima Bangi
Alisema mtuhumiwa Lungula Pina yeye kabla ya kukamatwa siku hiyo alikuwa
akituhumiwa kujihusisha na kulangua
Bangi na kuisambaza katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi na Mikoa ya
jirani
Na Mtuhuhumiwa
Agustino yeye amekuwa akijishughulisha
na kilimo hicho cha Bangi kwa muda mrefu sasa na
amekuwa ni miongoni mwa wakulima maarufu kijijini hapo wa madawa hayo ya kulevya
Kidavashari
alisema mbali ya kukamata Bangi hiyo na
mbegu zake jeshi la polisi liliweza kuteketeza
kwa moto Bangi za watuhumiwa
zaidi ya eka moja ambayo ilikuwa bado ipo shambani ambayo ilikuwa bado
haija vunwa
Alisema jeshi la polisi Mkoa wa Katavi lanaendelea na
msako usio na kikomo ili kuwabaini watu wengine ambao
wanajishughulisha na kilimo na
kuuza madawa ya kulevya Katika wilaya zate za Mkoa huu
0 comments:
Post a Comment