Home » » Akamatwa na ngozi ya Chui

Akamatwa na ngozi ya Chui


N a Walter Mguluchuma
Mpamda
Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi  linamshikilia Chelehani Kulwa 33 mkazi wa kijiji cha Kapanga Tarafa ya Mwese Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kukamatwa na nyara za serikali ngozi ya chuwi
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari alisema  mtuhumiwa alikamtwa  hapo Agosti 1 mwaka huu majira ya saa tisa na nusu alasiri  nyumbani  kwake  akiwa na ngozi hiyo ya chuwi
Kamanda Kidavashari alisema  mtuhumiwa alikamatwa na nyara hiyo ya Serikali kufuatia taarifa zilizolifikia jeshi la polisi  kuwa mtuhumiwa huyo  amekuwa akijishughulisha na uwindaji haramu na amehifadhi ndani ya nyumba yake ngozi ya chuwi
Baada ya taarifa hizo kutoka kwa raia wema jeshi la polisi lilianza  uchunguzi  wa kumfuatilia mtuhumiwa huyo  kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho    cha Kapanga
Kidavashari alieleza kuwa ndipo siku hiyo ya tukio polisi  walipokwenda kumpekua mhuhumiwa  Chelehani  nyumbani kwake na kumkuta na ngozi ya chuwi  yenye thamani ya shilingi  milioni  5.670,000 kinyume  cha sheria
Alisema mtuhumiwa baada ya mahojiano  na jeshi la polisi alikiri kumiliki nyara hiyo ya Serikali kinyume na taratibu za sheria ya nchi
Upelelezi wa tukio hili umeisha kamilika na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani mapema wiki ijalo ili aewze kujibu shitaka la kukamatwa na nyara za serikali kinyume cha sheria ya Jamhuri ya  muungano wa Tanzania  ambayo  inakataza mtu binafusi kumiliki nyara za Serikali

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa