na walter mguluchuma mpanda katavi
POLISI mkoani
Katavi inamshikilia mkazi wa kijiji
cha Itetemya , Tarafa ya Karema
wilayani Mpanda , Masanja Kulwa (23) akituhumiwa
kumuua mkewe wa ndoa Nyingi Shida (21) kwa
kumnyonga kisha kumfunga na
kipande cha chandarua na na kumninginisza mrtini .
Inadaiwa chanzo
cha mauaji hayo
ni wivu wa kimapenzi
ambapo mke alikuwa akimtuhumu mumewe mara kwa mara kuwa
alikuwa na mahusiano ya
kimapenzi na mwanamke
mwingine kijijijini humo
Kwa mujibu wa
Kamanda wa Polisi mkoni Katavi Dhahiri
kidavashari mumewe wa marehemu huyo
inadaiwa alimfanyia ukatili huo
mkewe huu baada ya kuchukizwa na
kitendo cha mkewe huyo
kwenda kumfokea mwanamke ambaye
inadaiwa kuwa ni ‘ mpenzi ‘ wake.
Kamanda Kidavashari aliongeza kuwa
mtuhumiwa baada ya
kuvunja shingo la mkewe alimfunga na kipande cha
chandarua chandarua shingoni
mwake na kumning’iniza mtini
mita 70 kutoka
nyumbani kwao .
Aliongeza kuwa tukio hilo
lilitokea Julai 31 , mwaka
huu saa
sita usiku kijijini humo
baada ya wanandoa hao
kuzozana na kushutumia
ambapo marehemu anadaiwa kukasirishwa
na tabia ya
mumewe kuwa na mahusiano na mwanamke
kijijini humo..
Kidavashari alidai kuwa siku moja
kabla ya tukio hilo kutokea marehemu
akiwa amejifunga ‘kibwebe” alikwenda nyumba kwa mwanamke
mwezake kijijini humo usiku
na kumwonya aache kuwa na mahusiano
ya kimapenzi na mumewe .‘.
Inadaiwa
ndipo wanandoa hao
waliposhindwa kuelelewana na kuanza kupigana ambapo
alfajiri ya siku iliyofuata
wapiti njia waliuona mwili wa
marehemu ukiwa unaning’inia mtini
akiwa ameshakufa ambapo mara moja
walimsaka mshutumiwa na kumkamata
kisha kumkabidhi katika Kituo
cha Polisi .
Kwa mujibu
kidavashari uchunguzi wa
kitabibu alibainisha kuwa shingo
la marehemu huyo lilikuwa limevunjika huku
akiwa na majeraha
yaliyotokana na kipigo katika
sehemu mbalimbali za mwili wake
ambapo alionekana kuwa
na majeraha makubwa mdomoni .
Kamanda Kidavashari
amedai kuwa mtuhumiwa huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani
wakati wowote mara tu baada
ya uchunguzi wa awali
wa shauri hilo
la mauaji kukamilika
0 comments:
Post a Comment