Na Walter Mgulucuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja aitwaye Simoni Kalaba( 56) Mkazi wa kijiji
cha Kakese Wilaya ya Mpanda ameuwawa kwa kukakatwa na panga na watu wasio
julikana wakatika akielekea nyumbani
kwake kwa mke wake bibi mgogo
Afisa mtendaji wa
kata hiyo ya Kakese Lubeni Kasomo alisema marehemu huyo ameuwawa na watu
hao wasio fahamika usiku wa kuamkia jana jirani
na nyumba ya mke mdogo wa marehemu
Alisema siku hiyo
ya tukio Simoni alishinda nyumbani kwake kwa mke mkubwa kijijini hapo
na alipo fikia majira ya saa tatu usiku alimuaga mke mkubwa pamoja na
watoto
wake kuwa anakwenda kulala kwa mke mdogo na wataonana siku ya kesho
yake asubuhi
Afisa mtendaji wa
kata alieleza kuwa ndipo ilipo fikia
jana majira ya saa 2 Asubuhi mwanae mkubwa
mtoto wa mke mkubwa ambae
walikubaliana kuonana nae mapema asubuhi alipo fika nyumbani kwa mama yake na
kumkosa alipoamua kumfuata nyumbani kwa mama yake mdogo
Alisema mwanae
huyo alipofika nyumbani kwa mke mdogo wa maremu
alimuuliza mama yake mdogo kama
baba yake bado yupo hapo nyumbani kwake na alijibiwa na mke mdogo wa
marehemu kuwa baba yake toka jana kutwa nzima hajaonekana kwake ingawa
siku hiyo alikuwa anaratiba ya kulala kwa mke mdogo
ambae ni yeye
Mke mdogo
alimweleza kijana huyo wa marehemu
kuwa atayeye ameshitushwa na
kitendo cha mume wake kutolala kwake na ndio maana nimewatuma watoto wakamwangalie kwa mama yao mke mkubwa wa Simoni
Afisa Mtendaji
Lubeni Kasomo alieleza baada ya majibu hayo ya mke mdogo mwanae na marehemu
aliamua kurudi nyumbani kwa mke mkubwa ndipo alipo kuwa ajiani aliona sati la
baba yake likiwa pembeni ya barabara uku
likiwa na damu huku baba yake akiwa
aonekani
Hari hiyo ilimfanya asogee kidogo kwenye
kichaka na ndipo alipo
mwona baba yake akiwa amelala kichakani huku akiwa na majeraha kichwani
na damu zikiwa zimetapakaa na kupelekeaapige mayowe ya kuomba msaada
ambapo majirani walipo fika katika eneo
hilo na kumwinua Simoni walikuta tayari ameisha kufa
Kamanda wa Polisi
wa mkoa wa Katavi Dhairi Kidavashari amethibitisha kutokea kwa mauwaji ya mtu
huyo Katika kijiji cha Kakese na jesi
hilo linaendelea na cchunguzi wa tukio
ili kuweza kuwabaini waliohusika au
kuhusika na mauwaji ya mtu huyo
0 comments:
Post a Comment