Home » » Afa baada yakunywa gongo nyingi kupita kiasi bila kula chakula‏

Afa baada yakunywa gongo nyingi kupita kiasi bila kula chakula‏


Na  Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mwananchi wa Mtaa wa Mpanda Hotel  Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi Aloyce  Alfred Sali (32) amefariki dunia baada ya kunywa pombe aina ya Gongo  kupita kiasi bila kula chakula
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  alisema kifo cha mtu huyo kilitokea hapo juzi  majira ya saa nane na nusu usiku  nyumbani kwa marehemu katika mtaa huo ambako alikuwa amepanga chumba
Kwa mujibu wa kamanda huyo mwili wa marehemu ulikutwa ndani ya chumba chake  ukiwa umelala chumbani  juu ya kitanda  ambapo marehemu alikuwa akiishi kwenye chumba hicho peke yake
Alieleza siku hiyoya tukio marehemu aliondoka hapo alipo kuwa amepanga  majira ya saa saba mchana na kuelekea kwenye kilabu cha kuuza pombe za kienyeji inayo milikiwa na mtu anaye tambulika kwa jina la Mwandosya ilipo katika mtaa huo wa Mpanda Hotel na kuanza kunywa pombe hiyo ya Gongo
Imeelezwa kwamba marehemu  alirejea nyumbani kwake aliko kuwa amepanga  chumba majira ya saa tano na nusu  na aliwakuta wapangaji wenzake wameisha lala usingizi
Kamanda Kidavashari alieleza kuwa siku iliyo fuata wapangaji wenzake  walipo ona imefikia majira ya saa sita mchana mwenzao hakuwa ameamka  ndipo walipopata wasiwasi  na kufuatilia kwa karibu chumbani kwake  walibaini  marehemu alikuwa ameisha fariki dunia
Alisema  wapangaji wenzake baada ya kubaini kifo cha mpangaji mwenzao  walitowa taarifa kwa majirani ambao walifika katika eneo hilo na kisha walitowa taarifa kwa jeshi la polisi Wilaya ya Mpanda ambao waliwasili muda mfupi katika eneo hilo
Kamanda  Kidavashari  alieleza kuwa uchunguzi  watukio hilo umeonyesha chanzo cha kifo  cha marehemu Aloycekimetokana na kunywa pombe nyingi aina ya Gongo  pasipo kula  chakula chochote kile
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti  katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda  na utakabidhiwa kwa ndugu  tayari kwa shughuli za mazishi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa