na walter nguluchuma mpanda katavi
WATU wawili wamekufa
katika matukio tofauti mkoani
Rukwa akiwemo mtoto Ester Sangu
(3) kufariki dunia baada ya nyumba yao
kuteketezwa kwa moto huku ndugu zake wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya.
Kaimu Kamanda wa
Polisi mkoa wa Rukwa,Longinus Tibishubwamu , amesema kuwa
tukio hilo lilitokea kijijini
Lunyala wilayani Nkasi Julai 29 , mwaka
huu saa kumi na mbili jioni na
kuwataja watoto waliojeruhiwa baada ya
nyumba yao hiyo kuteketezwa na moto kuwani pammoja na
Samweli Sangu (4) na Isaya Sangu (6)
Alisema kuwa tukio hilo la
kuungua moto nyumba hiyo lilitokea
wakati marehemu na ndugu zake
hao wawili walioachwa ndani ya nyumba hiyo na
bibi yao alipoenda kismani kuchota maji huku
akiacha amtenga
maharagwe kwenye jiko lililokuwa likitumia kuni huku
wakichochoea moto ili yaize haraka
.
“Baada ya
kuawacha pale nyumbani wajukuu wake
hao watatu moto wa kuni uliokuwa
ukiwaka kwa
nguvu jikoni cheche zake ziliruka na
nyasi zilizoezekwa kwenye paa la
nyumba hiyo zilishika moto na kuteketeza nyumba hiyo
“ alisema
Kwa mujibu wa Kaimu
Kamanda huyo majirani waliwahi katika eneo la
nyumba hiyo na kufanikiwa
kuwaokoa watoto hao wawili.
Katika tukio lingine
lililotokea kijijini Kipa mwambao mwa Ziwa
Rukwa wilayani Sumbawanga ambapo John mwabulambo
(49) alifariki dunia baada ya
kushambuliwa na kundi la wavuvi wakimtuhumu kuiba nyavu za
kuvulia samaki yenye thamani ya Sh 200,000.
Kwa mujibu wa
Tibishubwamu mtuhumiwa aitwaye Andrew Namboti
(32) ananashikiliwa kwa mahojiano na Polisi akihusishwa na tukio
hilo kwamba atafikishwa mahakamani mara tu
uchunguzi wa shauri lake hilo utakapokamilika.
0 comments:
Post a Comment