Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Watu wawili wamefikishw kizimbani mbele ya mahakama ya
Hakimu mkazi ya Wilaya ya Mpanda kwa
tuhuma za kukamatwa na bunduki ya kivita
aina ya SMG ikiwa na magazine moja na risasi
21 za Smg.
Walio fikishwa
kizimbani mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi Chiganga Tengwa wa mahakama hiyo ya
hakimu mkazi ni Bosco Mpamgwa ( 48)
mkazi wa mtaa wa Mpanda hotel Mjini hapa na Frenk Sabuni ( 21) mkazi wa
kijiji cha Stalike Wilaya ya Mlel
Watuhumiwa |
Mwendesha
mashitaka Insipekita msaidizi wa polisi
Razalo Masemno aliiambia mahakama kuwa
washitakiwa hao wawili walikamatwa na bunduki hiyo aina ya Smg No BD17B804 huku
ikiwa na Magazine moja na risasi 21 za bunduki aina ya Sar na Smg
Aliieleza
mahakama kuwa watuhumiwa hao wawili walikamatwa hapo julai 20 mwaka huu majira
ya saa sita na nusu usiku huko katika Kijiji
cha Stalike Wilaya ya Mlele huku silaha hiyo ikiwa na namba tofauti ya
vifaa vilivyo tumika kutengenezea
bunduki hiyo
Mwendesha
mashitaka alisema mahakamani hapo
watuhumiwa walikamatwa kufuatia taarifa za sili
zilizotolewa na Raia wema kwa
jeshi la Polisi na Askari wa hifadhi ya
Taifa ya wanyama pori ya Katavi
Mwendesha
mashitaka aliendelea kuiambia mahakama kuwa watuhumiwa walikamatwa na askari
polisi kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya Taifa ya Katavi huku wakiwa na
bunduki hiyo huku mtuhumiwa Bosco
Mpangwa akiwa ameivaa huku akiwa ameifunika kwenye koti lake leusi
Watuhumiwa hao
walikuwa wakielekea hifadhi ya Taifa ya Katavi
kwa ajiri ya ujangili katika hifadhi hiyo mwendesha mashitaka alidai
kuwa watuhumiwa ni wazoefu wa maswala ya ujangili kwani wote wawili wanakabiliwa na kesi nyingine katika mahakama
hiyo walizo fikishwa nazo walishitakiwa kwa tuhuma za kukamatwa na nyara za
Serikal pia bunduki hiyo inadaiwa walikuwa wakiitumia kwa matukio ya uhalifu
Baada ya kusomewa
mashitaka hayo watumiwa hao wawili
walikana mashitaka hayo namwendesha mashitaka aliiomba mahakama
isitowe dhamana kwa watuhumiwa hao kwa kile alichoieleza mahakama watuhumiwa
kosa hilo sio la kwanza kufanya la nama hiyo
Hakimu mkazi
mfawidhi Chiganga Tengwa aliamulu
washitakiwa waende rumande hadi hapo Agosti 5 mwaka huu baada ya kushindwa
kutimiza mashariti ya mdhamana ambapo kila mmoja alitakiwa awe na wadhamini
wawili wenye mali zisizo hamishika
0 comments:
Post a Comment