Home » » James Mbatia apata mpinzani uchaguzi mkuu NCCR MAGEUZI

James Mbatia apata mpinzani uchaguzi mkuu NCCR MAGEUZI

Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Kamishina wa chama cha NCCR MAGEUZI wa Mkoa wa Katavi  Charles Makofila (37)  ambae ni mlemavu wa viungo vya mwili  amechukua  fomu  na kujaza  kugombea nafasi ya mwenyeki wa Taifa wa chama hicho nafasi ambayo inashikiliwa kwa sasa na James Mbatia 
Makofila

Makofila alichukua fomu hizo hapo  julai  19  katika ofisi za chama hicho  zilizopo katika mtaa wa kotazi  mjini  Mpanda  alizo kabidhiwa na katibu wa chama hicho wa  wilaya Rajab Makana
Akizungumza na waandishi wa habari hapo juzi  Makofila alieleza  kuwa  yeye ni mwanachama wa chama hicho   namba ya kadi yake ni AC077956 aliyo ikata mwaka 2000  na  shughuli zake yeye ni mfaya biashara maarufu wa katika kata ya Mpanda ndogo Tarafa ya Kabungu Wilaya ya Mpanda
Alisema ameamua kugombea nafasi hiyo  katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Oktoba  mwaka huu ili  aweze kupata nafasi hiyo ili aweze kukijenga chama hicha  ambacho ameona hakiendi sawa kwa sasa
Sababu nyingine aliyo mfanya agombee nafasi hiyo alisema kuwa  ameona viongozi wa sasa  hawasimamii vizuri mali za chama hicho  na wameshindwa kutatua migogoro  iliyopo ndani ya chama hicho kwa muda wa mrefu sasa kazi ambayo  yeye anawea kuifanya
Pia alisema  viongozi hao walioko madarakani  wamekuwa kwa muda wote wameshindwa kutembelea mikoani  ili waimalishe chama  na matokeo yake siku hadi siku chama hicho kinazidi kupoteza  umaarufu  Mikoani  hivyo endapo atachaguliwa  atahakisha anarudisha imani hiyo kwa  wanachama wa chama hicho ambao wameisha vunjika moyo
Kamishina huyo wa wa NCCR MAGEUZI  wa mkoa wa Katavi Charles Mkofila  katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010  chama chake  kilimweka  kuwa mgombea wa  nafasi ya ubunge wa jimbo la Mpanda vijijini  jimbo ambalo lilichukuliwa  na mgombea wa CCM Moshi Selemani Kakoso

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa