Home » » Wawili wakamatwa na silaha ya kivita

Wawili wakamatwa na silaha ya kivita

Bunduki ya kivita aina ya SMG ikiwa na magazini moja na risasi 21. Picha zote na Walter Mguluchuma
Watuhumiwa BOSCO MPANGWA (48) na Frank sabuni miaka (21) wakiwa katika kituo cha police mkoani Katavi baada ya kushikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za kukamatwa na bunduki ya kivita.
Kamanda wajeshi la police DHAHIRI KIDAVASHARI akionesha mbele ya waandishi wa habari bunduki ya kivita aina ya SMG yenye namba za usajili BD17B804 ikiwa na magazini moja na risasi 21 SMG/SR amabyo walikamatwa nayo watu wa wili.


Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Jeshi la  Polisi  Mkoa  wa Katavi kwa  kushirikiana   na Askari wa Hifadhi  ya Taifa  ya Katavi  wamefanikiwa kuwakamata watu wawili  wakiwa na silaha bunduki ya kivita aina ya SMG ikiwa  na risasi 21 na magazini moja 

Kamanda  wa Polisi wa Mkoa wa Mkoa wa katavi Dhahiri Kidavashari  aliwataja watuhumiwa hao wawili  kuwa ni Bosco Mpangwa ( 48) mkazi wa mtaa wa Mpanda hoteli Wilaya ya Mpanda na Frenk Sabuni( 21) mkazi wa Kijiji cha Sitalike Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Kidavashari alisema watuhumiwa hao walikamatwa mnamo hapo Julai 20 mwaka huo majira ya saa sita  na nusu usiku  katika eneo la Kijiji cha Sitalike  wilayani Mlele na silaha hiyo aina ya SMG  iliyo tengenezwa na sehemu tatu yaani mwili wa bunduki hiyo ikiwa na Namba BD 17B 804 Cockingi Handle  yenye namba  H 7092 na Lisiva  gamba la juu  namba 685ikwa na risasi 21 za bunduki aina ya SMG na SAR

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia taarifa  za siri  zilizotoka kwa Raia wema walizo zifikisha kwa askari wa jeshi la polisi  na askari wa hifadhi ya wanyama poli ya Katavi na baada ya taarifa hizo ndipo walipo weka mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhimiwa hao  wakiwa katika eneo la shule ya msingi Sitalike

Kamanda Kidashari alieleza watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na silaha hiyo pamoja na risasi zikiwa katika magazine moja  ambapo mtuhumiwa Bosco  Mpangwa  alikuwa ameivaa silaha hiyo akiwa ameifunika ameifunika kwa koti lake jeusi

Watuhumiwa hao  walikuwa katika harakati za kuelekea katika hifadhi ya Taifa ya Katavi kwa ajiri ya shughuli za ujangili  katika hifadhi hiyo  na watuhumiwa  hao ni wazoefu  wa maswala ya ujangili  na pia silaha hiyo imekuwa ikitumika katika matukio mbalimbali ya uharifu  mkoani Katavi 

Alisema watuhumiwa hao pia wanakabiliwa na kesi mbili  za mwaka 2008 na 2012 walizo shitakiwa kwa kosa la kuhujumu  uchumi  baada ya kupatikana na nyara za Serikali ambazo kesi hizo zipo zinaendelea katika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Mpanda 

Kamanda Kidavashari  ametowa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi kufannya kazi  halali ambazo zitakazo waletea kipato  badala ya kujishughulisha  na uharifu  kwani  Mkoa wa Katavi sio sehemu  ya kufanyia uharifu  na kwa jinsi  jeshi hilo lilivyo jiimalisha  mtu yoyote atakaye fanya uhalifu lazima  akamatwe
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa