Home » » Bingwa wa mbio za baiskeli mbaroni kwa mauaji

Bingwa wa mbio za baiskeli mbaroni kwa mauaji



Mtuhumiwa wa mauaji Masaga chales (36)

Walter Mguluchuma, Mpanda
JESHI la Polisi  mkoani Katavi  linamshikilia bingwa  wa mashindano  ya  mbio  za baiskeli Masaga Charles (36) kwa tuhuma za kufanya mauaji ya kinyama mwaka   jana  Jijini  Arusha.
Mtuhumiwa  huyo ambaye kwa  zaidi ya miaka 15 amekuwa akishiriki  katika mashindano  ya mbio  za  baiskeli   katika Mikoa ya Tabora, Shinyanga na Mwanza, Oktoba mwaka jana na aliibuka mshindi katika mshindano ya baiskeli Arusha na kujinyakulia sh. 800,000.
Kwa  mujibu  wa Kamanda  wa Polisi  wa Mkoa wa Katavi , Dhahiri Kidavashari mtuhumiwa  huyo  ambaye  ni  mkazi wa Kijiji  cha Chilalo Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza anatuhumiwa  kumua Moshi  Bella (44) mkazi wa Kijiji cha Karema kwa kumkatakata na panga  kichwani na shingoni.
Taarifa zaidi zaidi zinasema mwanamichezo huyo alitekeleza mauaji hayo baada kulipwa shilingi  milioni tano alizopewa kabla ya kutekeleza kosa hilo.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  alisema tukio hili la mauwaji ya kinyama lilitokea mnamo julai 21 mwaka huu majira ya saa tisa alasiri katika kijiji cha Kabange  Kata ya Simbwesa   Tatafa ya Kabungu  Wilayani
kidavashari alisema mtuhumiwa kabla ya kufanya mauwaji hayo  alikwenda kuonana na marehemu  na kujifanya anataka marehemu amuuzie shamba mazungumzo ambayo yalifanyika hapo  julai 20 mwaka huu nyumbani kwa Salumu Kajimba  ambae  ni ndugu wa marehemu  na alikuwa amefikia hapo akitokea Kijijini kwake Karema
Alisema mtuhumiwa na marehemu walikubaliana  kuuziana shamba ambalo ni mbuga ya mpunga ekari mbili na kila heka walikubaliana kuuziana kwa kila heka kwa shilingi laki tatu kwa  heka  na baada ya makubaliano hayo mtuhumiwa alimwahidi  marehemu kuwa atarejea siku inayo fuata kwa ajili ya kutoa fedha za malipo  ya ununuzi wa shamba hilo
Kidavashari alieleza  siku iliyo fuata mtuhumiwa Masaga  Charles alifika nyumbani kwa Salumu Kajimba  kwa ndugu wa marehemu  mnamo majira ya saa tisa alasiri  kwa bahati mbaya alikuta  marehemu Moshi  Bella  akiwa ameelekea mbugani kwenye kisima  kwa ajiri ya kuoga
Mtuhumiwa  baada ya kuambiwa marehemu amekwenda shambani  alimuaga Salimu  Kajimba na mkewe Salumu  kuwa anamfuata huko huko mbungani
Kamanda Kidavashari alisema marehemu  hakuonekana tena nyumbani hapo toka alivyo waaga kuwa anakwenda kuoga kisimani wala mtuhumiwa aliyemfuata huko hakurejea  hadi hapo mwili wa marehemu  ulupo kutwa kwenye mbuga akiwa  ameuwawa kwa kukatwa na panga sehemu za shingo kwanyuma  na kichwani
Alisema jeshi la polisi  lilipata taarifa  toka kwa raia wema kuhusiana na mauaji hayo  na ndipo lilipoanza kumfuatilia mtuhumiwa  na polisi walifanikiwa kumkamata akiwa katika eneo la mtaa wa Makanyagio mjini hapa
Baada ya mtuhumiwa  kukamatwa alikiri  kuhusika na mauaji hayo  na alisema  alifanya hivyo  kwa kuwa  alitumwa na mtu  mmoja aliye tambulika kwa jina moja  tuu la Ndedesela  mkazi wa Kijiji cha Iroba Tarafa ya Kabungu Wilayani hapa.
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote  ili aweze kujibu tuhuma za mauwaji  ya kuuwa kwa kutumia panga


Na Katavi yetu

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa