washiriki wa semina ya manunuzi wakifuatilia mada
zinazowasilishwa na mtoa mada hayupo pichani.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa ukaribu mada
iliyokuwa ikiwasilishwa na mtoa mada toka PPRA kwa watumishi wa halmashauri za
mpanda na mlele mkoani katavi semina iliyofanyika ukumbi wa Halmashauri ya
wilaya ya Mpanda ulioko idara ya Maji
Mwezeshaji toka PPRA Bi Moza Hamisi akiotoa mada juu
uandaji na uandikaji wa mikataba kwa
wazabuni kwa washiriki wa semina ya manunuzi ambao hawaonekani pichani.
washiriki wakiwa kwenye vikundi vya majadiliano kujadili
mada zilizokuwa zimewasilishwa na watoa mada baada ya kugawanywa kwenye vikundi
ili kupima uelewa kama kweli kile wanachofundishwa wamekielewa.
Na Kibada
Kibada -Mpanda.
Watumishi
wa Halmashauri za wilaya ya Mpanda na Mlele wamepigwa Msasa kuhususiana na
sheria ya manunuzi na taratibu zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kuandaa mikataba
kwa ajili ya kufanya manunuzi ya serikali ili kuepuka kufanya kazi kinyume na
maadili taratibu na sheria za manunuzi ya serikali.
Semina
hiyo ambayo imefadhiliwa na Halmasahauri ya wilaya ya mpanda inalenga kuwajengea
uelewa watumishi kuhusu masuala ya mikataba na manunuzi ya mali za serikali hususani
wale ambao ni wenye dhamana ya suala la manunuzi kwenye idara za serikali.
Mkuu wa
kitengo cha manunuzi Halmashauri ya wilaya mpanda Bi Ashura Kang’ombe alisema wameamua
kuwaita wataalamu kutoka PPRA ili kutoa semina ya siku tano iliyofanyika kwenye
ukumbi wa Halmashauri ya wilaya yam panda na kushirikisha watumisha zaidi ya 30
wakiwemo wakuu wa Idara wakuu wa Vitengo, na wasaidizi wao pamoja na watumishi
wa kawaida na walio wengi kutoka kitengo cha manunuzi na wale wa fedha.
Watoa
mada katika semina hiyo Moza Hamisi na Hirtrudice Jisenge wamezungumzia
umuhimu wa sheiria za manunuzi hali iliyowafanya washiriki kusikiliza kwa
umakini na muda wote.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa semina hiyo kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
ya wilaya ya Mpanda Patrick Mwakyusa ambaye pia ni mwanasheria wa Halamsahuri
ya Mpanda alioneshwa kufurahishwa na semina hiyo na kueleza furaha yake kwa
wawezeshaji na kutoa shukurani za pekee kwa PPRA Kwa jinsi walivyoonesha moyo
wa kwajari watumishi wa Halmashauri yake kwa kuwaletea semina inayohusiana na
manunuzi kitendo ambacho alisema ni cha kuigwa na mamlaka nyingine.
0 comments:
Post a Comment