Mkuu wa mkoa
katavi Dr Rajabu Rutengwe akisoma taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge Jum
Ally simai hapo jana kwenye kijiji cha ifumbura katika makazi ya wakimbizi wa
mishamo mara baada ya kukabidhiwa mwenge wa uhuru na mkuu wa mkoa kigoma issa
machibya.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Miradi 36 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni
2 inatarajiwa kufunguliwa wakati wa
ziara ya mbio za mwenge zilizo anza jana katika mkoa wa Katavi
Hayo yalisemwa hapo jana na mkuu wa mkoa wa
Katavi Dr rajabu Rutengwe katika risala
aliyo isoma mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge Juma Simai
mara baada ya kukabidhiwa mwenge
na Mkuu wa Kigoma katika kijiji cha cha Ifumbula kilichoka katika makazi ya wakimbizi ya Mishamo
Dr Rutengwe alisema katika fedha hizo wahisani wamechangia kwenye miradi hiyo
kiasi cha shilingi milioni 751,505,135
serikali kuu shilingi milioni
466,055,712 na Halmashauri zake
mbili zimechangi jumla ya shilingi milioni 632,622.962 nakufanya jumla ya
thamani ya pesa ya miladi hiyo ni
shilingi Bilioni 2.044,059,281
Aliitaja miradi itakayo
funguliwa kuwa ni miradi wa kisima
Kilefu katika kijiji cha Isenga mrari wa
upimaji wa viwanja katika kijiji
cha Vikonge ofisi ya afisa tarafa wa Kabungu mradi wa vyumba viwili vya madarasa
katika kijiji cha vikonge ujenzi wa ghala la kuhifadhi chakula katika
kijiji cha mpembe na ujenzi wa jengo la
utawala katika shule ya sekondari ya Ilandamilumba miradi ambayo ipo katika halmashauri ya
wilaya ya mpanda
Miradi ya Halmashauri ya
mlele ni ujenzi wa nyumba ya askari
na ufunguzi wa mitaa katika
kijiji cha Kibaoni ujenzi wa ofisi ya kata Usevya . uzinduzi wa mashine ya kukoboa na
kusaga Kibaoni na ujenzi wa mabweni yenye mahitaji maalumu
Pia aliitaja miradi itakayo
funguliwa katika Halmashauri ya mji wa Mpanda kuwa ni ghala la mazao
ya chakula kituo cha kurushia
matangazo ya radio. ujenzi wa ofisi ya Kata ya Ilembo uzinduzi wa barabara ya lami yenye ulefu wa
kilometa moja katika stendi ya mabasi
na ujenzi wa madarasa matatu ya kidato cha tano katika shule yasekondari
ya Rungwa
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge
Juma Simai aliwataka wakazi wa Mkoa wa Katavi waache
tabia ya kuchoma moto misitu kwa ni
kuharibu mazingira
Kauli hiyo aliitowa
kufuatia kutoridhishwa na wakazi wa mkoa wa Kigoma kuchoma moto
misitu sehemu kubwa ya misitu iliyoko
katika barabara ya kutoka Kigoma KUELEKEA Katavi
0 comments:
Post a Comment