Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi
limemkamata Ramadhani Issana .(32) mkazi wa Tabata Dar es
salaam kwa tuhuma za kumwibia Ameriko Bejarano GALUZA
Raia wa Nchi ya Mexico mkazi wa Mkoa wa Arusha laptop
moja aina ya Toshiba na nyaraka zake muhimu za kusafiria ikiwemo pasipoti
yake pamoja na pesa tasilimu tsh 200,000 kwenye nyumba ya kulala
wageni ya mjini hapa
Kaimu Kamanda wa jeshi Mkoa wa
Katavi Joseph Myovela alisema mtuhumiwa alikamatwa hapo jana majira
ya saa kumi jioni katika mtaa wa Makanyagio mjini hapa baada ya kuwa amefanya
wizi huo
Alisema siku hiyo ya tukio
mtuhumiwaRamadhani alikuwa amepanga katika nyumba moja ya
kulala wageni na Raia huyo wa Mexico ambaye ni mfanya
biashara wa madini katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Mijela iliyoko
katika mtaa wa Majengo B mjini hapa
0 comments:
Post a Comment