Na Kibada Kibada- Mpanda
Jeshi la polisi
Mkoa wa Katavi linamsaka Dickson Petro
mkazi wa Kijiji cha Mwamkulu Kata ya Kakese wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumuuwa mke wake kwa kumkata na kitu chenye ncha kali kichwani .usoni,na kwenye mikono yake yote
baada ya mwanamke huyo kukataa kuishi na mumewe
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
alimtaja mwanamke aliye uwawa na mumewe
kuwa ni Solile Elikana (35) mkazi wa kijiji hicho cha
Mwamkulu tukio hilo la mauwaji ambalo lilitokea hapo julai 15 mwaka huu majira
ya saa nne usiku nyumbani kwa marehemu
Alisema chanzo cha kifo cha mwanamke huyo kilitoka na ugomvi wa wanandoa
hao hao wawili uliotokea hapo julai 12 mwaka huu na kusababisha mwanamke huyo kukataa kuishi
na mumewe mbele ya kikao cha baraza la
serikali ya kitongoji cha Mwamkulu
Marehumu huyo
aliamua kumshitaki mumewe kwenye baraza hilo la serikali ya kijiji baada
ya mumewe kumpiga na kumsababishia
majeraha sehemu ta uso wake kitendo
ambacho kilimuudhi marehemu baada mumewe
kumtuhumu mkewe kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine kijijini
hapo
Alisema baada ya mwanaume huyo kushitakiwa kwenye baraza
hilo aliamua kwenda kwa mwenyekiti wa
kitongoji aitwaye Laulian Ngalu ili
aweze kuwasululisha lakini marehemu alikataa hari ambayo ilimfanya mwenyekiti huyo
aitishe kikao cha serikali ya kitongoji
kwa lengo la kuendelea kuwapatanisha
Hata hivyo katika kikao hicho marehemu alikataa kata kata kuendelea kuishi na mumewe
na kisha aliamua kwenda kuchukua nguo zake
na vyombo vyote walivyo nunua na
mume wake waligawana licha ya mume kumwomba marehemu waedelee kuishi
pamoja lakini marehemu aligoma
Kidavashari alieleza kuwa
baada ya kugawana vyombo hivyo
mtuhumiwa akuonekana tena kijijini hapo
kwa muda wa siku tatu toka walivyo achana na marehemu
Alieleza kuwa
ndipo siku hiyo alipo onekana
mtuhumiwa Dickson palikuwa na mkesha wa harusi kijijini hapo na marehemu ni miongoni mwa walioshiriki sherehe hiyo
kamanda Kidavashari
alieleza ndipo ilipo ilipotimia majira ya saa nne usiku marehemu aliamua kurudi nyumbani kwake na alipo fika karibu na nyumba yake
alishambuliwa na mume wake huyo kwa kumchoma
na kitu chenye ncha kari hadi kufa hapo na kisha kutokomea kusiko julikana
Wananchi walianza kutafuta mtuhumiwa
katika eneo hilo lakini hakuweza kupatikana licha wanakijiji hao kumsaka usiku kucha na katika vijiji vya jirani
Kamanda Kidavashari alisema jeshi la polisi linaendelea kumsaka mtuhumiwa ili atakapo kamatwa afikishwe kwenye vyombo
vya sheria na ametowa wito kwa wananchi
wa Mkoa wa Katavi kuwa na utaratibu wa
kuhakikisha kila mkazi anakuwa na anwani inayo tambulika ili anapo fanya
uharifu aweze kupatikana kwa urahisi
0 comments:
Post a Comment