Home » » KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AZINDUA MRADI WA MAJI WA SH.MILION 48.4

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AZINDUA MRADI WA MAJI WA SH.MILION 48.4


Na Walter Mguluchuma-Mpanda.
Wananchi wa Kijiji cha Tupindo Kata ya Mbede wilayani Mlele wameondokana na tatizo la maji lililokuwa likiwakabili kwa muda mrefu baada ya Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Juma Ali Simai  kuzindua mradi wa  kisima kirefu cha maji chenye thamani ya  ya shilingi milioni 48.4.
Uzinduzi wa Mradi huo ulifanyika  hapo jana na katika kijiji hicho na kuhudhuriwa na mamia ya na  wananchiya wananchi na Vijiji vya Jirani 
 Akisoma Taarifa ya Mradi,  Kaimu Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Respesius Leo alisema Mradi huo ambao umegharimu kiasi cha shilingi 48,400,000 milioni ulianza kujengwa mwaka 2012.
 Kati ya fedha hizo Halmashauri ya wilaya ya Mlele ilitoa kiasi cha shilingi 47.8 milioni,  wananchi wa Kijiji cha Tupindo walichangia  kiasi cha shilingi laki sita 600,000 fedha zote zilizotumika kwa ajili ya kuchimba kisima, ununuzi wa Tanki,ujenzi wa uzio,ujenzi wa kibanda cha  umeme  wa  jua (Sola Power),
Kaimu mwandisi huyo alisema  awali wananchi wa kijiji hicho  walikuwa wakilazimika   kusafiri umbali wa zaidi ya kilometa tano kwenda kutafuta huduma ya maji katika kijiji cha jirani
Alieleza kwenye risala hiyo  kuwa mbali ya huduma za  kibinadamu maji hayo  pia yatasaidia kwa ajili ya kunyweshea maji mifugo na bustani za mboga
Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho  Jojina  Katumbo alipo  ulizwa na kiongozi  wambio za mwenge Kitaifa  aeleze  namna  ya walivyo upokea mradi huo alisema mradi huo umekuwa ni mkombozi kwa wakazi wa kijiji hicho
Alisema  wanawake wa kijiji hicho wataondokana  na adha ya kuamka usiku wa manane  kwa ajiri ya kwenda kutafuta maji katika kijiji cha Usevya ambapo wakati mwingine walikuwa wakihatarisha usalama wa maisha yao
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa Juma Ally Sumai aliwataka wakazi wa kijiji hicho kuulinda na kuutunza  mradi huo
Aliwaeleza  mradi huo  waufanye uwe mradi endelevu  ambao utakao wawezesha  kuweza kuibua mradi mwingine kupitia pesa watakazo kuwa  wanazipata kupitia maji hayo watakayo yauza kwa bei ya shilingi  ishirini kwa ndoo moja
mwisho

    

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa