Home » » MAJAMBAZI WAPORA MAMILIONI NA KUUWA MFANYABIASHARA, WANNE WASHIKILIWA NA POLISI‏

MAJAMBAZI WAPORA MAMILIONI NA KUUWA MFANYABIASHARA, WANNE WASHIKILIWA NA POLISI‏

Na  Walter Mguluchuma

Mpanda
 Watu watano wanaosadikiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha mbili bunduki  aina ya SMG  wamemuwa kwa kumpiga  risasi  mbili tumboni  Juma  Mabula ( 36) mfanyabiashara wa Bariadi Shinyanga  na  kumpola  mamilioni ya  fedha  ambazo kiasi chake hakija fahamika  na kumjeruhi  kwa kumpiga  risasi mbili  tumboni Cosmas  Michael ( 28)  mfanya biashara wa Bariadi Shinyanga  na kumpora fedha   tasilimu milioni tatu
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi  Dhahiri Kidavashari  alisema tukio hili  lilitokea  juzi majira ya  saa mbili  usiku  katika kijiji  cha  Itunya  kata  ya Kapalamsenga  Tarafa ya Karema  wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi
Alisema majambazi hao  kabla ya kufanya tukio hilo  waliwavamia  Adolfu John (20 ) na kumpora  fedha  tasilimu Tsh 4, 000, 000/=  na Richard Charles  (25)   alimporwa  Tsh 5,000,000/=  ambao ni wafanya biashara na wakazi  wa  Kijiji  cha Kakese  Wilaya  ya Mpanda
Kidavashari alieleza  kuwa  wafanya biashara hao  walikuwa  wamekwenda kijijini hapo kwa lengo  la kununua zao la mpunga   linalopatikana kwa wingi kwenye kijiji hicho  na ndipo walipo patwa  na tukio hili
Alisema katika eneo la tukio hilo  liliokotwa ganda moja  la risasi   aina ya bunduki  ya SMG  lililotumika likiwa karibu  na mwili wa marehemu  Juma Mabula
Baada ya jeshi la polisi kupata taarifa lilifika katika eneo hilo  la tukio  na waliendesha msako mkali  na kuwakamata watu wanne  kuhusiana na tuhuma  za tukio hilo 
Kamanda Kidavashari aliwataja  watu hao wanao  shikiliwa na polisi  kuwa ni Mussa Mathias  (36),  Ngusa Tola  (37),  na Shinde  Jiyaago ( 34)  wote wakazi wa  kijiji  cha Nkuswe Tarafa ya Karema wilayani hapa na  Doto  Kayungilo  (25)  Mkazi wa kijiji  cha Mnyamasi Tarafa ya Kabungu
Alisema  majeruhi Cosmas  Michael  ambaye amelazwa katika Hospital ya Wilaya  ya Mpanda   anaendelea kupata matibabu na  hali yake inaendelea vizuri
Kamanda Kidavashari amewataka wananchi wa Mkoa wa Katavi  kuwabaini wageni wanaofika kwenye maeneo yao  na kutoa taarifa  kwa Jeshi la Polisi  za kuwaarifu  watakao wabaini  au  kuwatilia shaka watuhumiwa  ili waweze kukamatwa  kabla ya kutenda tukio

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa