Na Walter Mguluchuma
Mpanda
jeshi la polisi Mkoa
waKatavi linawashikilia watu watano kwa
tuhuma za kapatikana na vinywaji
aina juice Grand malt na pipi
zikiwa zimechanganywa madawa ya kulevya
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari
aliwataja waliokamatwa kuwa ni
Halid Bukela (38) mkazi wa Area C
Dodoma, Mayala Udembi( 45) mkazi wa mtaa wa Kigamboni Mpanda, Adulofu Kajuna (35) mkazi wa
Nyamagana Jijini Mwanza, Lucas Damiani (24) na
Elias Daudi (34 ) wote wakazi
wa Wilaya ya Urambo Mkoa wa Tabora.
Watuhumiwa hao walikamatwa
juni 5 majira ya saa 10
jioni katika Mtaa wa Majengo B’
Wilayani Mpanda wakiwa na
pipi moja juice mbili
na Grand Malta moja
ambazo zilikuwa zimechanganywa
madawa ya kulevya ambapo katika
tukio hilo walikamatwa wahumiwa
wawili Halidi na Maloda
Kidavashari alisema
watuhumiwa walikamatwa kufutia taarifa
ambazo zilikuwa zimelifikia jeshi la polisi kuwa watumiwa wanajihusisha na vitendo
vya utapeli na wanawalevya watu kwa madawa ya kulevya na kisha
wanawaibia mali zao
Alisema baada ya watuhumiwa
kukamatwa na kuhojiwa na Polisi walibaini kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakishirikiana
na wenzao ambao
walikuwa katika Kijiji cha Kakese
na ndipo Polisi walipo fanikiwa kuwakamata watu hao watu
Watuhumiwa hao ambao
ni Adolofu Lucas na Elias huku wakiwa na pipi inayodhaniwa kuwa na dawa
za kulevya
Kamanda Kidashari alisema
watuhumiwa hao wote watano bado
wanaendelea kushikiliwa na jeshi la
polisi kwa mahojiano zaidi na watafikishwa Mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika
Mkoa wa Katavi umekuwa
ukikabiliwa na matukio mbali mbali
ya utapeli hivi karibuni kutokana
na kuongezeka kwa wafanya biashara
wanaotoka nje ya Mkoa huu kwa
ajili ya kununua mazao ya Nafaka aina ya mpunga,
mahindi na ufuta
0 comments:
Post a Comment