Home » » AFA BAADA YA KUNYWA POMBE YA KIENYEJI YENYE SUMU‏

AFA BAADA YA KUNYWA POMBE YA KIENYEJI YENYE SUMU‏

Na Walter Mguluchuma
Katavi
Mtu Mmoja  Ngusa  Solea  (32) Mkazi  wa Kijiji cha Matandalani  Tarafa ya Nsimbo  amekutwa amekufa baada ya kunywa pombe ya kienyeji  aina ya Komoni  inayosadikiwa kuwa na sumu
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  alisema  tukio la kifo cha mtu huyo kilitokea  hapo juzi majira ya saa  tatu asubuhi
Alisema  Ngusa  siku hiyo alikutwa akiwa amefariki  dunia  nje ya nyumba  iliyo kuwa ikiendelea kujengwa Pagara  jirani  na nyumba ya  Anisety Matongo  huku  mwili wake  ukiwa  unatokwa na damu puani
Kidavashari  alieleza kuwa   usuku wa  tukio hilo  marehemu alionekana akinywa pombe  ya kienyeji  aina   komoni  nyumbani  kwa Anisety Matondo  mpaka usiku wa manane
Marehemu  hata hivyo   haikufahamika aliondoka saa ngapi   hapo alipo kuwa akinywa pombe  na ndipo  siku iliyo fuata  majira ya saa tatu asubuhi  alipo kutwa kwenye pagara akiwa ameisha  kufa
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi alisema  chanzo cha kifo  hicho  kinadhaniwa  kuwa ni  marehemu alikunywa  alikunywa pombe  ambayo ilikuwa na sumu
Alieleza mpaka sasa  hakuna mtu  au watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo   na jitihada za kubaini chanzo cha kifo  na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea
Alisema jitihada  za  kumtafuta Anisety Matondo  aliko kuwa akinywa pombe marehemu  zinaendelea  kwani  Anisety   alitoka kijijini hapo  mara baada ya kugundua  kuwa marehemu  Ngusa amefariki

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa