Home » » Auwawa akiwa chumbani kwake amelala‏

Auwawa akiwa chumbani kwake amelala‏

Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Mtu mmoja  Mkazi wa kijiji   cha Kasekese Tarafa ya Mwese  wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi  Anton  David ( 45)   ameuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani  na watu wasiojulikana
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidavashari  alisema tukio hilo lilitokea hapo jana   majira ya saa  nne usiku nyumbani kwa marehemu huyo
Alisema  marehemu alikutwa     ndani ya chumba chake  muda huo wa saa nne usiku  akiwa ameisha kufa  huku mwili wake ukiwa  umelala kitandani
Baada ya majirani kuuchunguza mwili  wa marehemu  walimkuta akiwa na  majeraha makubwa kichwani  yaliyo tokana na kupigwa na kitu  kizito  sehemu ya kichwa chake
Kamanda Kidavashari ameeleza kuwa jeshi la polisi mkoa wa Katavi linamshikiia mtu mmoja  aitwaye  John Mwanandota  (35) mkazi wa kijiji hicho cha Kasekese kuhusiana na tukio hilo
Jeshi la polisi  mkoa wa Katavi  limetowa wito kwa  wananchi  waendelee   kushirikiana na  jeshi la polisi  katika kupambana  na uharifu   katika maeneo yao  kwa kuimarisha  mfumo  wa ulinzi shirikishi  na ulinzi  jirani  ili  kuweza  kuwabaini  na kuwakamata  watu  wanaotenda  uharifu  katika  maeneo yao  ili waweze kufikishwa kwenye vyombo   vya sheria .

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa