Home » » KIJANA WA MIAKA 32 KIZIMBANI KWA KUMBAKA NA KUMRAWITI KIKONGWE WA MIAKA 90‏

KIJANA WA MIAKA 32 KIZIMBANI KWA KUMBAKA NA KUMRAWITI KIKONGWE WA MIAKA 90‏


Na walter Mguluchuma
Mpanda
Mkazi wa kijiji cha Bulembo makazi ya wakimbizi ya Katumba
wilayani Mlele Mkoa wa Katavi Sindebula Msagi (32) amefikishwa
kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya ya Mpanda
kwa tuhuma za kumbaka na kumlawiti mwanamke mwenye umri wa
miaka 90
Mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Ally Mbwijo aliiambia
mahakama hiyo hapo juzi mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa
mahakama hiyo Chiganga Tengwe kuwa mshitakiwa alitenda kosa
hilo hapo desemba 22 mwaka jana majira ya saa 8 usiku nyumbani
kwa kikongewe huyo.
Alisema siku hiyo ya tukio mshitakiwa Sindebula alifika
nyumbani kwa mama huyo na kuvunja mlango na kisha aliingia
ndani ya nyumba ya mama huyo ambae alikuwa ni mgonjwa wa kupooza
mguu wa kulia na mkono wa kulia kisha alimbaka na kumlawiti
kwa nguvu mama huyo
Pamoja na mama huyo kumsihi mshitakiwa asimfanyie kitendo hicho
alimweleza kuwa umri wake ni mkubwa hasitahili kufanyiwa hivyo
lakini mshitakiwa hakujali ombi la mama huyo bali aliendelea
kumfanyia unyama kikongewe huyo licha ya kupiga mayowe ya kuomba
msaada kwa majirani hakuweza kufanikiwa kutokana na nyumba aliyo
kuwa akiishi kuwa mbali na majirani
Mwendesha mashitaka aliendelea kuiambia mahakama hiyo ambayo
ililazimika kwenda kusikilizia kesi kwenye eneo la tukio
kutokana na hari ya mama huyo kuwa katika hari mbaya ya
kiafya kuwa mshitakiwa aliendelea kumfanyia unyama mama huyo
mpaka usingizi ukampata na kisha kulala ndani ya chumba cha mama
huyo
Alieleza ilipofikia majira ya saa 12 asubuhi ndipo mama huyo alipo
weza kufungua dirisha na aliweza kumwona mtu mmoja aitwaye Ashabola
Elly aliye kuwa akipita jirani ya nyumba yake ndipo alimwonyesha
ishara ya kumwita kwa kutumia vidole ili aweze kufika kumpatia msaada
Mwendesha mashtaka alisema baada ya Ashobola kuingia ndani alimkuta
mshtakiwa akiwa amelala chini na ndipo alipoweza kumtambua ila
hakuweza kumuamusha kutokana na tabia yake ya ukorofi hivyo
ilimlazimu akimbie kwenda kutoa taarifa kwa majirani .
Majirani waliweza kufika katika eneo hilo huku wakiwa na viongozi wa
kijiji hicho hata hivyo walikuta mshtakiwa amekwisha amka na
kutokomea.
Alisema polisi walifanikiwa kumkamata mshtakiwa muda mfupi baada ya
kuwa ametoka kwenye nyumba hiyo na katika maelezo yake ya awalai
mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo kutokana na kile alichodai
kilisababishwa na pombe nyingi ya kienyeji aliyokuwa amekunywa aina ya
Kayoga
Taarifa ya daktari aliyemfanyia uchunguzi mama huyo imeonyesha
kuharibiwa vibaya sehemu zake za siri na haja kubwa , katika kesi hiyo
upande wa mashtaka una mashahidi wanne na mshtakiwa hana shahidi
yoyote.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga aliamuru mshtakiwa kwenda Rumande hadi
hapo March 28 mwaka huu kesi yake itakapaosikilizwa.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa