Home » » DC MLELE AWALALAMIKIA WATUMISHI WA IDARA YA MALIASILI NA MAZINGIRA‏

DC MLELE AWALALAMIKIA WATUMISHI WA IDARA YA MALIASILI NA MAZINGIRA‏


NaWalter Mguluchuma
Katavi
Mkuu wa  Wilaya ya Mlele   Kanali  Gemela  Lubinga  amewalaumu watumishi wa Idara ya Maliasili  na Mazingira wa Wilaya  hiyo  kwa kutokuwa  waaminifu katika majukumu yao ya  kazi

Kauli hii aliitowa hapo juzi  mbele ya waandishi wa habari  wakati  alipokuwa akizungumza nao  ofisini kwake akiwaelezea  namna ya shughuli mbambali  za utekelezaji wa maendeleo zilizo fanyika katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita na kutekelezwa  wilayani  Mlele.

Alisema idara ya Maliaslili  inaonekana kutokuwa na watumishi waanifu   na hari hiyo  imekuwa  ndio  chanzo  cha watu  kuvuna  mbao  kwenye  maeneo yasiyo  sitahili   na  kusababisha uharibifu wa mazigira

Alieleza kuwa yeye Mkuu wa wilaya mwishoni  mwa wiki  iliyopita  alifanya msako  kwenye maeneo ya Game Reserve ya Mlele na  kufanikiwa  kukamata watu wakiwa  wanachana mbao  mwenye  maeneo  hayo na  aliweza kukamata mbao  3000 za aina ya mninga

Alifafanua kuwa  Serikali  imekuwa ikitoa pesa kwa  watumishi wa idara ya Maliasi  kwa ajiri  kulipa  wakafanye  kazi  za  kuwasaka  watu  wanao  vamia maeneo ya misitu  lakini kazi hiyo  wamekuwa hawaifanyi ipasavyo

Kama mimi  kwa muda wa siku moja  nimeweza  kukamata watu na mbao  hizo wao  huwa wako wapi.

Matokeo yake serikali imekuwa ikiingia gharama kubwa ya pesa na matumizi ya gari kwa ajili ya watumishi wa maliasili wanapokwenda kufanya msako lakini inaonekana kazi hiyo haifanyiki kwa ufanisi alisema Lubinga

Alisema  kutokana na watumishi wa  wa idara hiyo  kutokuwa waaminifu  kuna weza  kukaisababishia  wilaya hiyo  na Nchi kwa ujumla  hasara  itokanayo na uharibifu wa mazigira

Alieleza kuwa  maeneo  mingi   ya hifadhi za  misitu    katika wilaya ya Mlele yamevamiwa  na  wachana mbao ambao baada ya kuzichana zimekuwa zikisafirishwa kinyemelana wafanya biashara hiyo kuyoka mikoa yaMwanza Moshi   Tabora  na Dares salam

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa